Habari za Punde

Mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria kwa viongozi wa dini yafanyika Pemba

 MRATIBU wa mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria kwa viongozi wa dini kisiwani Pemba, Safia Saleh Sultan, akieleza kwa ufupi juu ya mafunzo hayo yaliofanyika mjini Chake chake na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni mwanasheria kutoka wizara ya katiba na sheria Mohamed Ali Maalim katikati na Mratibu wa ZLSC Pemba Fatma Khamis Hemed, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  WASHIRIKI wa mafunzo ya kuwatambulisha kazi za wasaidizi wa sheria ambao ni viongozi wa dini, wakifuatilia mada kadhaa zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mafunzo hayo, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na kufanyika mjini Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba)

 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akielezea mada ya dhana ya wasaidizi wa sheria, kwenye mafunzo ya viongozi wa dini yaliotayarishwa na ZLSC na kufanyika mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Mohamed Hassan Ali, akitoa mada kwenye mafunzo ya viongozi wa dini, yalioandaliwa na ZLSC na kufanyika mjini Chake chake, kushoto ni mratibu wa mafunzo hayo Safis Saleh Sultan, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.