Habari za Punde

Mgombea Urais Kupitia Chama cha AFP Mhe Said Soud Said Arejesha Fomu ya Urais wa Zanzibar.


Mgombea Urais kupitia Chama cha AFP Mhe Said Soud Said, akiwasiliana na jamaa wakati akiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar kurejesha Fomu leo mchana. 
Mgombea Urais wa Chama cha AFP Mhe Said Soud Said akiwa na viongozi wa Chama chake wakiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko hoteli ya Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kurejesha fomu yake ya kugombea Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa AFP akiwa ukumbi wa Afisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakati wa hafla ya kurejesha fomu akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, hayopo pichani. 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha.S.Jecha akipokea Fomu za kugombea Urais kwa Mgombea wa Chama cha AFP Mhe. Said Soud Said, alipofika Afisi za Tume ziliko katika hoteli ya bwawani Zanzibar kurejesha fomu zake kwa mchakato ya Tume. 

Mgombea Urais kupitia Chama cha AFP Mhe Said Soud Said akikabidhi fedha za malipo ya Fomu ya Urais wa Zanzibar shilingi milioni mbili kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha.S.Jecha. 

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe.Jecha.S.Jecha akiweka saini kukamilisha zoezi la mgombea kurejesha fomu kwa wakati uliowekwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Nae Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg Salum Kassim Ali akizihakiki fomu za Mgombea
Mgombea Urais kupitia Chama cha AFP Mhe Said Soud Said akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu zake za kugombea Urais wa Zanzibar kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.