Mgombea Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma Mhe Issa Mohammed Zonga akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar zilioko katika hoteli ya bwawani kwa ajili ya kurejesha fomu zake za kugombea Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Chama cha Sauti ya Umma akiwa na viongozi wa Chama hicho wakisubiri kurudisha fomu yake Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma akionesha mkoba wake wenye fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar akiwaonesha waandishi wa habari kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar. alipofika Afisi za Tume ya Uchaguzi kurejesha fomu zake.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jecha.S.Jecha akipokea fomu za mgombea Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma Mhe Issa Mohammed Zonga, hafla hiyo imefanyika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mhe Issa Mohammed Zonga akionesha fedha za kulipia Fomu yake ya Urais shilingi milioni mbili kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mhe Issa Mohammed Zonga akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha kwa ajili ya malipo ya fomu ya urais wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akisaini fomu za Mgombea kupitia Chama cha Sauti ya Umma Mhe Issa Mohammed Zonga baada ya kuzikabidha kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment