Habari za Punde

Mnara wa Miaka 50 ya Mapinduzi Wazinduliwa leo na Dk Shein

 Muonekano wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi ukionekana wakati wa mandhari ya usiku katika bustani ya michezani kisonge ukiwa katika maandalizi ya uzinduzi wake uliofanyiuka asubuhi hii na kuzinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.

Haiba ya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka Hamsini ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 inavyoonekana baada ya kumalizika kujengwa hapo katika Majumba ya Maendeleo Michenzani Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein akikata utepe kuashirika kuufungua Rasmi Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Michenzani Mjini Zanzibar.
Mshauri wa Ujenzi wa Mnara wa wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar Mhandisi Abdul Aziz akimpatia maelezo Rais wa Zanzibar Dr. Shein wakati akiukagua Mnara huo baada ya kuuzindua rasmi.
 
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akiangalia mandhari ya Mji wa Zanzibar katika chombo maalum { Darubini } wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar Michenzani baada ya Kuuzindua rasmi.
Mandhari ya Bustani ya Michenzani iliyomo ndani ya eneo la Mnara linavyoonekana kwa juu ya Mnara wa Kumbu kumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.