Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akizungumza na viongozi na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe leo kabla ya kukabidhi msaada wa shuka 176 kusaidia wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela akiongea na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe kabla ya kupokea msaada wa mashuka ya wagonjwa wilayani humo leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE).
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akikabidhi msaada wa shuka 176 kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela (kulia) leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na uhaba wa mashuka.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokelo(kulia) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige kwa pamoja wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE kwenye wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(wa pili kushoto), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokelo(kushoto ) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige (kulia) na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Kisarawe wakielekea lilipo jengo la wodi ya wazazi.
Wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe wakifurahia msaada wa mashuka yaliyotolewa kwa wagonjwa na Chuo cha Elimu ya Biashara, CBE leo. Picha/Aron Msigwa - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment