Habari za Punde

Uzinduzi wa kampeni za ubunge CCM jimbo la Mkoani

 VIJANA Asha na Sada wakisoma utenzi wakati wa uzinduzi wa kampenzi za Ubunge CCM Jimbo la Mkoani, kampenzi hizo zilizofanyika huko katika Uwanja wa Black Wizard Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mkoani, wakiwa na picha za mgombea Ubunge jimbo la Mkoani Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa kampenzi za Ubunge jimbo hilo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Mkoani Omara Makame akizungumza na wanaCCM wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Ubunge za CCM Jimbo la Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MGOMBEA ubunge Jimbo la Chake Chake Mbaraka Said Rashid, akitoa salamu za wananchi wa Chake Chake wakati wa uzinduzi wa kampenzi za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkoani kupitia Profesa Makame Mnyaa Mbarawa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Wawi kisiwani Pemba Daudi Khamis Juma, akiwasisitiza wananchi kumpigia kura ya ndio wagombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:John Makufuli na Mhe:Dk Ali Mohamed Shein kuendelea tena kuwa madarakani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mkoani kisiwani Pemba, Mhe:Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akicheza mziki na wanachama wa CCM mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha Black Wizard Chokocho Mkoani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mkoani Mhe:Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa CCM jimbo la Mkoani huko Chokocho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mkoani Mhe:Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akizindua sare za wananchi na wanachama wa CCM, kwa ajili ya kampenzi za jimbo hilo, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa CCM jimbo la Mkoani huko Chokocho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

MGOMBEA uwakilishi jimbo la Mkoani kisiwani Pemba Mmanga Mjengo Mjawiri, akiwaonesha wanaCCM wa Jimbo la Mkoani Ilani ya CCM ambayo ndio mongozo wao katika utekelezaji wa maendeleo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.