Mgombea Urais kupitia Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid, akiwasili Afisi za Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya kurejesha Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar, akishindikizwa na Wanachama wa Chama hicho.
Mgombea wa Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid akiwa na Viongozi wa Chama chake katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC zilioko bwawani hoteli.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha akipokea fomu za Mgombea wa Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid alipowasilisha fomu zake baada ya kukamilisha taratibu zote alizotakiwa kufanya ili kupata kuchaguliwa kugombea Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid akikabidhi fedha za kulipia fomu ya kugombea Urais shilingi milioni mbili kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha baada ya kukabidhi fomu zake za kugombea nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha.S.Jecha akisaini fomu za Mgombea wa Chama cha CHAUMMA Mhe. Mohammed Masoud Rashid, baada ya kuzipokea na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe Salum Kassim Issa akizipitia fomu hizo.
Mgombea Urais kupitia Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid akizungumza na waandishi wa habari na kutowa shukrani kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kuitaka kuwa huru katika Uchaguzi Mkuu na kusisitiza atafanya Kampeni bila ya matusi na kwa amani.
Mgombea Urais kupitia Chama cha CHAUMMA Mhe Mohammed Masoud Rashid akitoka Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar baada ya kukabidhi fomu zake kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Mhe Jecha.S.Jecha baada ya kukamilisha taratibu zote za ujazaji wake.
No comments:
Post a Comment