Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ndg.Salum Kassim Ali akitoa neno la utanguzlizi kuhusu wajibu wa wagombea wa Uchaguzi katika warsha ya siku moja kwa wagombea wa Uwakilishi yenye lengo la kuongeza ufahamu juu ya maadili ya Uchaguzi na kuibua hatua madhubuti katika kuimarisha Amani ndani ya kipindi hiki cha Uchaguzi, warsha hiyo ilifanyika tarehe 09/09/2015 Ukumbi wa Hoteli ya Hifadhi Zanzibar.
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mh. Ayoub Bakar Hamadi akifungua warsha ya Wagombea wa Uchaguzi iliyofanyika tarehe 09/09/2015 Ukumbi wa hoteli ya Hifadhi Chake Chake Pemba, warsha hiyo ilikuwa na lengo la kuongeza ufahamu wa maadili ya Uchaguzi na kuibua masuala ambayo yanaweza kuzuia kuwepo kwa Uchaguzi wa Amani


No comments:
Post a Comment