Habari za Punde

Wapiga kura waanza kupatiwa shahada zao za kupiga kura ZEC

DSC03464
Wapiga kura kutoka shehia ya Mtoni kidato wakiwa katika kituo cha ugawaji wa shahada za kupigia kura kwa ajili ya kupatiwa shahada zao tarehe 28/09/2015.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeanza kazi ya ugawaji wa Shahada za kupigia kura kwa shehia zote za Unguja na Pemba kwa ajili ya Uchaguzi mkuu Octoba 25 mwaka huu.
DSC03468
Karani wa kituo cha Ugawaji wa shahada za kupigia kura shehia ya Bububu (skuli ya kidichi) akihakiki risiti ya mpiga kura kabla ya kumpatia shahada yake tarehe 28/09/2015.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inagawa Shahada za kupigia Kura kwa Wapiga Kura wapya walioandikishwa mwaka 2015 na 2013 na wale ambao wameandikishwa 2009/2010 na hawakuchukua shahada zao.
Aidha, wapiga kura waliohamisha taarifa zao,waliofanya masahihisho ya taarifa katika shahada zao na waliopoteza shahada za kupigia kura wataruhusika kwenda kuchukua shahada zao.
DSC03462
Karani wa kituo cha Ugawaji wa Shahada za kupigia kura Shehia ya Mtoni Kidato akimkabidhi Mpiga kura Shahada yake baaada ya kufikika kituoni huko tarehe 28/09/2015.
Kazi ya Ugawaji wa Shahada za kupigia kura itafanyika katika vituo vya kujiandikisha kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 28-30/09/2015 ambapo zoezi hilo litafanyika katika Afisi za Wilaya za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.