WANANCHI na WanaCCM wa Zanzibar wametakiwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kwani ndio chama pekee kinachoweza kusimamia amani na utulivu nchini
sambamba na kuimarisha maendeleo kwa wananchi wote bila ya ubaguzi.
Viongozi wa CCM Zanzibar waliyasema hayo
leo huko katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliofanyika uwanja wa
Urafiki, Jimbo la Shaurimoyo, Mkoa wa Mjini Magharibi uliohudhuriwa na maelfu
ya wanaCCM na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar
kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein.
Viongozi hao wa CCM walipata fursa ya
kusalimiana na wananchi pamoja na WanaCCM waliohudhuria katika mkutano huo na
kuwaeleza haja ya kuwachagua viongozi wa
CCM ili waendelee kuwaletea maendeleo sambamba na kusimamia amani na utulivu
iliyopo.
Dk. Hussen Mwinyi ambaye ni Waziri wa
Ulinzi na (JKT) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipata fursa ya
kuwasalimia wananchi na wanaCCM na kupata fursa ya kumpongeza na kumshukuru Dk.
Shein kwa kuendeleza amani na utulivu nchini na kusema kuwa Wizara ya ulinzi imerizika
na hatua hiyo kwa Zanzibar.
Alisema kuwa ana matumaini makubwa hatua
hiyo itaendelezwa hiyo ni kutokana na kuwa CCM itaendelea kuongoza na kuwataka
wananchi na WanaCCM kuwachagua viongozi wa CCM ili amani na utulivu izidi kudumu.
Akieleza juu ya ajira katika vyombo vya
ulinzi na usalama, Dk. Mwinyi alisema kuwa kuna idadi maalum kwa kila mwaka
iliyotengwa kwa ajili ya vijana wa Zanzibar na kuwataka wananchi kutopotoshwa
na hilo.
Idadi hiyo inaletwa na kugaiwa kwa
kupitia Wilaya zote za Zanzibar na kuahidi kuwa hatua hiyo itaendelezwa ili
vijana wengi wazidi kupata ajira katika vyombo hivyo vya ulinzi.
Aliwataka wanaCCM kutobweteka na kuwataka
wasikae majumbani siku ya kupiga kura na badala yake waende kupiga kura na kuwachagua
viongozi wote wa CCM ili kuendeleza amani na utulivu iliyopo na kuimarisha maendeleo.
Maendeleo yote yaliopo nchini yameletwa
na CCM hivyo kuna kila sababu ya kuwachagua viongozi wa CCM ili kuendeleza
maendeleo hayo yaliofikiwa.
Nae Balozi Amina Salum Ali, alieleza kuwa
alisema kuwa CCM haikotayari kutoa uongozi kwa chama chengine chochote kwani
chama hicho ndicho pekee kinacholeta maendeleo na kuwajali wananchi wa rika
zote, hali zote na jinsia zote.
Alieleza kuchukizwa na maneno ya viongozi
wa upinzani kuwa hakuna maendeleo nchini na kusema kutokana na maendeleo
makubwa yaliofikiwa katika nchi za Afrika hatua hiyo ilimfanya Rais wa Benki ya
Dunia kusema kuwa maendeleo yanayopatikana hivi sasa yatapelekea mnamo mwaka 2020
umasikini kupungua kwa kiasi kikuhwa katika nchi za bara la Afrika.
Balozi Amina alisema kuwa maendeleo ya kiuchumi
ndio yanayoimarisha uchumi na hatua hiyo ndio iliyofikiwa na Zanzibar chini ya
uongozi wa Dk. Shein ambapo uchumi umekuwa kwa asilimia 7.
Alisema kuwa katika uongozi wa Dk. Shein
mafanikio makubwa yamepatikana na kuwataka wananchi na wanaCCM kumpa kura Dk.
Shein kwani amefanya mambo mengi na kueleza kuwa endapo watamchagua ataendeza
palipofikia.
Nae Balozi Seif Idd aliwaambia wanaCCM wa
Unguja na Pemba waanze kupamba kwani sababu za kushinda zipo kwani CCM imeamua
na kusisitiza matawi yote yaanze kupambwa kwa ajili ya kusherrehekea ushindi wa
CCM
Alisema kuwa cha cha CCM kitazidi kuimaimarika
na kukua kwani ndicho kitakachokuwa kikiongoza Serikali baada ya kupata ushindi
mkubwa katika uhaguzi wa mwaka huu.
Alisema kuwa wafusia wa chama cha CUF ni
wabaguzi kwani hivi karibuni walifukia kaburi na kukataa kuzikwa maiti mwenye
asili ya kimasai huko Kiwengwa kwa vile anatoka bara na kupelekea maiti ya
marehemu huyo ikawie kuzikwa huku akisema kitendo hicho cha kumbagua maiti si
cha kiungwana.
Alisema kuwa iwapo wakipewa nchi wanaweza
kuwabagua Wazanzibari wote kwani tayari wameshaanza ubaguzi.
Haroun Ali Suleiman ambaye ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi
wa Umma akizungumzia suala la ajira alisema kuwa tayari Sera ya Ajira
imeshapitishwa na hivi sasa mipango imeshakamilika kwa kuandaa ajira mbali
mbali, na kueleza kuwa Dk. Shein ameanzisha Mfuko Maalum wa Uwezeshaji kwa
ajili ya kuwasaidia vijana waliokosa ajira Serikalini.
Waziri Haroun alisema kuwa Serikali
imeanzisha kituo maalum katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji na Ajira kwa lengo la
kupanua sekta ya ajira.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka
minne Dk. Shein ameweza kufanya mabadiliko ya mishahara mara tatu.
Akieleza mafanikio katika sekta ya elimu,
Haroun alisema kuwa wanafunzi wa darasa la sita hivi sasa wataingia kidato cha
nne moja kwa moja na kueleza mipango ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika kuangalia maslahi ya waalimu.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai
Ali Vuai, alirudia kauli ya Dk. Shein ya kuongeza mshahara wa kima cha chini
kufikia Shilingi laki tatu katika mwaka wake wa kwanza atakapoingia madarakani
na kusisitiza kuwa hizo ndio ahadi za Dk. Shein zinazotekelezeka.
No comments:
Post a Comment