Habari za Punde

Mkutano wa kampeni wa CCM jimbo la Shaurimoyo


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika uwanja wa Urafiki,jimbo la Shaurimoyo katika wilaya ya mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiimba wimbo wa kuhamasisha wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zilizofanyika leo uwanja wa Urafiki jimbo la Shaurimoyo Wilaya ya mjini mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Kitaifa ya CCM  Balozi Amina Salim Ali  akitoa salam zake kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine waliohudhuria katika Mkutano wa  Kampeni za Uchaguzi zilizofanyika katika kiwanja cha mpira cha Urafiki jimbo la Shauri Moyo kilichopo Wilaya ya Mjini Unguja.

Mjumbe wa Kamati kuuya CCM na Makamo wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi akiwasalimia  wananchi na wanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi katika uwanja wa mpira Urafiki jimbo la Shaurimoyo Mjini Unguja leo.
 Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozana kuelekea katika uwanja wa Urafiki katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

 Watoto wakiwa wamevalia sare za Chama cha Mapinduzi walizopewa na Wazazi wao ili kukisherehekea Chama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Urafiki Jimbo la Shaurimoyo Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini wakati alipowasili uwanja wa Urafiki katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Shaurimoyo leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi  CCM  wakati alipowasili uwanja wa Urafiki Jimbo la Shaurimoyo leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zinazoendelea.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono Wanachama wa CCM na Wananchi  wakati alipowasili uwanja wa Urafiki Jimbo la Shaurimoyo leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zinazoendelea, (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakiimba wimbo wa Chama na Viongozi wengine  wakati alipowasili uwanja wa Urafiki Jimbo la Shaurimoyo leo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM zinazoendelea.
Vijana wa Chamacha Mapinduzi walipokuwa wakiimba maalum wa kuhamasisha  wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika leo katika uwanja wa Urafiki Jimbo la Shaurimoyo Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.