MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha
Wananchi CUF Mhe: Maalim Seif Sharif Hamad akivishwa koja, kabla ya kuzungumza
na mamia ya wanachama wa vyama vinavyounda UKAWA, uliofanyika Ditia Jimbo la
Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MJUMBE wa baraza kuu taifa la chama cha CHADEMA Janeth
Madadi Fussi, akitoa salamu zake kwa mamia ya wanachama wa vyama vinavyounda
UKAWA, kwenye mkutano uliofanyika Ditia, Jimbo la Wawi wilaya ya Chake chake
Pemba, na kuhutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF maalim Seif
Sharif Hamad, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
WANACHAMA wa CUF na wengine wanaounda UKAWA,
wakifuatilia hutuba ya mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF maalim Seif
Sharif Hamad, akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa majimbo ya
Chake chake na Wawi pamoja na wadi zake, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
KADA wa chama cha wananchi CUF bwana
Sanya akizungumza kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa Majimbo ya Chake chake
na Wawi na wadi zake, uliofanyika uwanja wa Ditia Jimbo la Wawi na kuhutubiwa
na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, maalim Seif Sharif Hamad,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akimnadi mgombea Udiwani wa wadi ya Tibirinzi Mohamed Hafidh
Ngwidi, kabla ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano
uliofanyika Ditia Jimbo la Wawi, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF maalims
Seif Sharif Hamad, akimnadi mgombea Ubunge Jimbo la Chake chake Yussuf Kaiza
Makame, kabla ya kuzungumza na wanachama wa chama hicho, kwenye mkutano
uliofanyika Ditia Jimbo la Wawi, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama
cha wananchi CUF Mhe: maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachamawa chama
hicho, kwenye mkutano wa kuwanadi wagombea wa nafasi mbali mbali wa majimbo ya
Wawi na Chake chake, mkutano huo ulifanyika Ditia Jimbo la Wawi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment