Mhe. Mahadhi J. Maalim Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
akizungumza wakati wa Mkutano wa Nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) wakati wa
mkutano wa Mawaziri wa Kundi hilo uliofanyia siku ya Alhamis hapa Makao Makuu
ya Umoja wa Mataifa. Nyuma ya Naibu
Waziri, ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu
wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan M. Mwinyu
Na Mwandishi Maalum, New York
Wakati kila
Nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa,
ikijianda kwa utekelezaji wa Ajenda 2030 ambayo inajikita zaidi katika kuondoa umaskini
pasipo kumwacha yeyote nyuma, sanjari na kuilinda Sayari Dunia. Tanzania
imehimiza haja na umuhimu wa nchi ambazo ziko
nyuma kimaendeleo ( LDCs) kuzungumza kwa kauli moja.
Ushauri huo umetolewa jana Alhamis na Mhe. Mahadhi Juma Maalim ( Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, wakati akizungumza katika mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama
wa LDCs uliofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, sambamba na majadiliano
ya jumla ya Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa.
Katika mkutano huu wa Mawaziri wa LDCs, Bangladesh ilikabidhiwa uenyekiti wa Kundi hilo kutoka kwa Benin inayomaliza muda
wake. Pamoja na Kuishukuru Benin kwa
kuliongoza kundi hilo vema wakati wa
uenyekiti wake Mhe. Naibu Waziri ameiahidi Bangladesh ushirikiano kutoka Tanzania.
“
Kundi letu linawachama
wengi, tutumie basi wingi wetu
kuhakikisha kwamba tunasukuma
mbele na kuteteta masuala yanayotuhusu
kwa kuzungumza kwa sauti moja wakati wa majadiliano na kuhakikisha
kuwa ajenda tunazosimamia kwa maslahi
yetu hazikwami.” Amesema Naibu Waziri
Aidha Naibu Waziri
Mahadhi, amelikumbusha kundi hilo kuwa moja
ya lengo kuu la kundi ni kuondoka katika kundi la nchi maskini na kuwa
nchi zenye uchumi wa kati.
“ Kwa bahati nzuri suala la kuondoa umaskini ni moja ya eneo
ambalo limepewa umuhimu wa kipekee katika Ajenda 2030, hivyo ni wajibu
wetu kama LDCs, kutumia fursa hii kwa
kuhakikisha kwamba, katika kipindi cha miaka 15 ijayo nchi nyingi katika kundi
letu zina-graduate na kuwa nchi zenye uchumi wa kati”. Amesisitiza.
Mhe. Naibu Waziri
amerejea kwa kusisitiza kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati
alipolihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, siku ya Jumanne, Kwamba utekelezaji wa Ajenda 2030
ndiyo changamoto iliyombele yetu kwa sasa na kwamba utekelezaji wake ukikwama,
LDCs ndizo zitakazo athirika zaidi.
Ni kwa sababu hiyo juhudi
za pamoja katika kuhakikisha utekelezaji wa
Ajenda 2030 ni mihimu na za lazima.
Kundi la Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo na kama
zinavyotambuliwa na Umoja wa Mataifa zipo 48
Ajenda 2030 ambayo
ilipitishwa wakati wa mkutano wa kilele wa kisiasa uliofanyia kwa siku tatu
hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa, ni Ajenda yenye malengo 17 ya maendeleo
endelevu yakichukua na nafasi ya Malengo
ya Maendeleo ya Milenia ambayo yanafikia
ukingoni mwaka huu wa 2015
Ajenda 2030 itaanza
kutekelezwa mwakani ( 2016 )na utekelezaji wake ni wa miaka 15
No comments:
Post a Comment