Habari za Punde

Taarifa ya Wizara kuhusu Mahujaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea jina la Bw. Khamis Juma Shamte hujaji kutoka Tanzania aliyefariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015. Kifo cha Bw. Shamte kinafanya idadi ya vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu nane (8) hadi sasa.

Aidha, Wizara imepokea jina la Bi Hawa Amrani Khamis aliyekuwa amepotea tangu siku ya ajali hiyo ambaye amepatikana akiwa mzima na aliweza kuungana na Mahujaji wengine na kurejea nyumbani tarehe 02 Oktoba, 2015.

Vile vile orodha ya majina ya majeruhi wote wa ajali ambao bado wapo hospitali imetolewa. Hadi sasa kuna Mahujaji wanne (4) wa Tanzania ambao wanaendelea kupatiwa

matibabu katika hospitali mbalimbali za Saudi Arabia na hali zao zinaendelea vizuri. Mahujaji hao ni Bi. Hidaya Mchomvu, Bi. Mahjabin Taslim Khan na Bw. Ahmed Abdalla Jusab. Pia, kuna mgonjwa mmoja ambaye aliugua tangu alipowasili Madina akitokea nchini anayeitwa Mustafa Ali Mchira ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Ansari Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Bw. Mchira hakujeruhiwa kwenye ajali ya mkanyagano.

Hadi kufikia tarehe 03 Oktoba, 2015, Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana naTanzania Hajj Mission na Vikundi vilivyopoteza Mahujaji umefanikiwa kupata majina ya Watanzania 32 ambao bado hawajapatikana. Orodha ya Majina na Vikundi vyao ni kama ifuatavyo:-

KIKUNDI CHA KHIDMAT ISLAMIYA

  1. Abdul Iddi Hussein
  2. Awadh Saleh Magram
  3. Burhan Nzori Matata
  4. Yussuf Ismail Yussuf
  5. Saleh Mussa Said
  6. Adam Abdul Adam
  7. Archelous Anatory Rutayulungwa
  8. Farida Khatun Abdulghani
  9. Rashida Adam Abdul
  10. Hamida Ilyas Ibrahim
  11. Rehema Ausi Rubbaga
  12. Faiza Ahmed Omari
  13. Khadija Abdulkhalik Said
  14. Shabinamu Ismail Dinmohammed
  15. Salama Rajabu Mwamba
  16. Johari Mkesafiri Mwijage
KIKUNDI CHA TCDO
  1. Alwiya Sharrif Abdallah
  2. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah
KIKUNDI CHA AHLU DAAWA
  1. Masoud Juma
  2. Issa Amiri Faki
  3. Juma Jecha Dabu
  4. Nassor Mohammed Hemed
  5. Mohammed Awadh Namongo
  6. Juma Yussuf Bajuka
  7. Said Habibu Ferej
  8. Khadija Hamad
  9. Rahma Salim
  10. Hadija Abdallah Sefu
  11. Farida Khamis
  12. Nuru Omar Karama
  13. Laila Manunga
  14. Saida Awadh

Zoezi la kuwatambua Mahujaji wa Tanzania ambao bado hawajaonekana linaendelea. Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha nyingine zipatazo elfu moja (1,000) kwa ajili ya kuangalia Mahujaji waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

05 Oktoba, 2015

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.