Habari za Punde

WanaCCM watakiwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 kuwachagua wagombea wa CCM

Na Maryam Kidiko –Maelezo                         

Wanachama wa chama cha Mapinduzi wametakiwa ifikapo tarehe 25,mwezi huu kwenda kwa wingi katika Vituo vya kupigia kura na kuwachagua wagombea wa chama hicho kuanzia Madiwani mpaka Maraisi.

Akizungumza na Wanachama wa chama cha Mapinduzi Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) January Makamba katika mkutano wa Jimbo huko Welezo wakati akiwanadi wagombea wa chama cha Mapinduzi Madiwani ,Wawakilishi na Wabunge.

Amesema endapo wakiwachagua wagombea wa chama hicho kuanzia ngazi ya chin mpaka ya juu bila ya kufanya makosa chama hicho  kitawaletea maendeleo wanachama wake katika nchi .

Aidha amesema kuwa Viongozi wa chama cha Mapinduzi ni viongozi makini na wanaozungumzia maendeleo katika Majukwaa na sio kuzungumza vitendo vya kuiharibu amani ya nchi.

Nae Saada Mkuya Salum anaegombania Ubunge Jimbo la Welezo kwa Tiketi ya CCM amesema endapo atapata ridhaa kutoka kwa Wananchi atahakikisha anarejesha matunda aliyopewa na chama cha Mapinduzi  kwa Wananchi wa Jimbo hilo.

Vile vile amesema Miundo mbinu katika Jimbo la Welezo ataiboresha nakuondoa tatizo kubwa la maji linalowakabili kwa muda mrefu ambalo halijapatiwa ufumbuzi  katika  Jimbo hilo.

Hata hivyo Saada amesema atashirikiana na Mamlaka husika na kuliondoa tatizo hilo pamoja na matatizo mengine yanayowakabili wananchi na kuwapatia vyanzo vya kujiajiri wenyewe .


Sambamba na hayo amesema kwakuwa yeye ni Mwanamke  anayajua Matatizo ya Wanawake ,kwakushirikiana nao atahakikisha anaviboresha Vikundi vya akina mama  ili waweze kujiendeleza kimaisha .

Amewataka Wananchi wa Jimbo la Welezo kumchaguwa katika kumpigia kura na kwakutoa mashirikiano yao ni wazi kuwa atapata ushindi katika Jimbo hilo na kuwa Mbunge na kuyatatua matatizo ya Wananchi .

Wakati huo huo Muwakilishi na Diwani wanaogombania Jimbo hilo wamesekuwa endapo watachaguliwa na wananchi watatoa ushirikiano mkubwa kwa Viongozi na Wananchi ili kuhakikisha Jimbo hilo ni Jimbo litalokuwa na Maendeleo Makubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.