Habari za Punde

Go For Zanzibar GOZA Yaikabidhi Vifaa Timu ya Ujamaa Academy

Katibu Mkuu wa Klabu ya Ujamaa Juma Khalfan akizungumza wakati wa ziara ya Ugeni kutoka Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya Go For Zanzibar (GOZA) ya Ujerumani walipofika katika klabu hiyo kupata maendeleo ya Vijana wa Ujamaa Soccer Academy kwa ajili ya kutoa vifaa kwa Vijana hao
Meneja Miradi wa GOZA  Mussa Khamis Baucha  kukabidhi vifaa kwa ajili ya Vijana hao na kuelezea  shughuli zinazofanywa na GOZA katika  Nyanja mbalimbali za kuinua Vijana katika maendeleo kutojihusisha na vitendo viovu, hafla hiyo imefanyika katika klabu ya Ujamaa rahaleo Unguja.kulia Mwenyekiti wa GOZA Antje Fleischer kutoka Ujerumani.
Meneja Miradi wa GOZA Mussa Khamis Baucha akiwa na mipira ya soksi baada ya kukabidhiwa na Uongozi wa Ujamaa.
Mwenyekiti wa Go For Zanzibar GOZA Antje Fleischer akimkabidhi mipira Katibu Mkuu wa Ujamaa Juma Khalfan nae akikabidhi mipira ya soksi ambayo ilikuwa ikitumiwa na Watoto katika kucheza mitaani ambayo hutumika kwa kuchezea watoto mitaani,hafla hiyo imefanyika katika klabu ya Ujamaa Rahaleo Unguja.katikati ni Meneja Miradi wa GOZA Mussa Khamis Baucha.
Mwenyekiti wa Klabu ya Ujamaa Ameir Makungu akitowa shukrani kwa Uongozi wa Go For Zanzibar  GOZA kwa ushirikiano wao kwa tamu ya Ujamaa kwa misaada yao mbalimbali wanayotoa kwa klabu hiyo kwa kuwaendeleza vijana wadogo katika kukuza kifya na vipaji.

katika maendeleo kutojihusisha na vitendo viovu, hafla hiyo imefanyika katika klabu ya Ujamaa rahaleo Unguja.kulia Mwenyekiti wa GOZA Antje Fleischer kutoka Ujerumani.

Mwenyekiti Go For Zanzibar  GOZA  kutoka Ujerumani Bi. Antje Fleischer akiwakabidhi zawdi ya Krismax Vijana wa Ujamaa Soccer Academy  ili kuweza kusherehekea sikukuu hiyo na mwaka mpya.katikati Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha.
Viongozi wa Go For Zanzibar GOZA  wakiwa katika picha ya pamoja na Vijana wa Ujamaa Soccer Academy nje ya klabu ya Ujamaa Rahaleo baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
Viongozi wa Timu ya Ujamaa Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa GOZA nje ya jengo la Klabu ya Ujamaa Rahaleo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.