Habari za Punde

Mama Samia alipohudhuria maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW)

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Msaidizi Mkoa wa Magharibi Kichama Zanzibar Suleiman Mzee (CHARAS) alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria ghafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria Ghafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akisalimiana na kumfahamisha wake zake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto  alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria Ghafla ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.