Habari za Punde

Mandhari ya Kisiwa cha Uzi, Zanzibar

 Kisiwa cha Zanzibar kina mandhari zenye kupendeza na zenye historia ya kipekee. 

Kutana na kamera ya mpiga picha anaechipukia Ismail Ishu alipofanya matembezi maalum ya kutembelea kisiwa kizuri cha Uzi.


Kisiwa hiki kinaweza kufikiwa kwa gari kwa kutumia njia hii iliyojengwa kwa mawe wakati maji yamekupwa na yanapojaa basi gari haiwezi kupita hapa mpaka maji yakupwe tena.

Wenyeji wameshaizoea hali hii na wanajua fika mwenendo wa bahari na kujipangia maisha yao
Wana wa Uzi wakiendelea kusukana kama walivyokutwa na mpiga picha anaechipukia Ismail Ishu wakati alipofanya ziara maalum kukitembelea kisiwa cha Uzi na kupata kumbukumbu za aina yake

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.