Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Jumanne Magembe kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki wakisubiri kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ikuli jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, kuwa Waziri wa Ujenzi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapishwa Mawaziri wapya walioteuliwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri waliohudhuria hafla hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Hamad Masauni (kulia) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri aliowaapisha leo Ikulu
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na Makamu wake Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakiwapongeza Mawaziri hao mara baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,leo Desemba 28, 2015. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment