AFISA Mdhamini wizara ya Elimu Pemba
Kitwana Salim Sururu akifungua mkutano wa siku moja, wa kutoa ushauri wa
kuliimarisha somo la uraia, mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Mkaguzi wa elimu Amour Rashid na kushoto
ni Afisa Mipango wa ZLSC Mohamed Hassan Ali, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAALIMU wa somo la uraia Kisiwani Pemba,
wakifanya kazi za makundi, kutoa changamoto na njia za ufumbuzi ili
kuliimarisha somo hilo, kwenye mkutano uliofanyika Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba mjini Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
BAADHI ya watendaji wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba na wanasheria wengine, wakielekea kisiwa cha
Fundo wilaya ya Wete, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya msaada wa kisheria
duniani, kwa kuwapa msaada wa kisheria wananchi wa shehia hiyo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
:
WATENDAJI wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wanasheria wa serikali na waandishi wa
habari wakiwa kwenye fukwe ya kisiwa cha Fundo wilaya ya Wete, kwenda kuwapa
wananchi msaada wa kisheria bila ya malipo, ikiwa ni maadhimisha ya siku ya
msaada wa kisheria duniani, (Picha na
Haji Nassor, Pemba).
MAOFISA wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakitoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa shehia
ya Fundo wilaya ya Wete, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya msaada wa
kisheria duniani, (Picha na Haji Nassor,
Pemba).
MWANDISHI wa habari kituo cha radio cha ZENJ FM Pemba
Berema Suleiman Nassor, akizungumza na mwananchi wa shehia ya Fundo wilaya ya
Wete, Omar Khamis Hamad (70) mara baada ya kupewa msaada wa kisheria,
uliotolewa na wanasheria walioungana na Kituo cha Huduma za Sheria Pemba,
kwenye maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WATENDAJI wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC pamoja na wanasheria wakirudi kisiwa cha Fundo wilaya ya Wete,
kwenye maadhimisho ya siku ya msaada wa kisheria, ambapo wananchi kadhaa
walipewa msaada huo bila ya malipo, (Picha
na Haji Nassor, Pemba).
MWANDISHI wa habari kituo cha radio cha ZENJ
FM Pemba Berema Suleiman Nassor, akizungumza na Mratibu wa Kituo cha Huduma za
Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed mara baada ya kuadhimisha
siku ya msaada wa kisheria, maadhimisho hayo yalifanyika Kisiwa cha Fundo
wilaya ya Wete Pemba, (Picha na Haji
Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment