Habari za Punde

Hafla ya kuadhimisha miaka 67 ya Uhuru wa Jamhuri ya India

Kaimu Balozi Mdogo wa India, Govind Sharan Gupta akisalimiana na Wananchi mbalimbali wenye asili ya India wanaoshi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuadhimisha miaka 67 ya Uhuru wa Jamhuri ya India iliyofanyika katika Ubalozi huo Migimbani mjini Zanzibar.

Wananchi mbalimbali wanaioshi Zanzibar wenye asili ya India wakiimba wito wa Taifa la India Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar.
Kaimu Balozi Mdogo wa India Govind Sharan Gupta akipandisha Bendera ya India kuashiria kuifungua sherehe ya Uhuru wa Jamuhuri ya India ya kutimiza miaka 67  katika Sherehe iliofanyka katika ubalozi huo Migombani Zanzibar

Wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo wakisherehekea baada ya kupandishwa Bendera ya Nchi ya India kuadhimisha miaka 67 ya Uhuru wa Jamhuri ya India iliyofanyika katika Ubalozi huo Migimbani mjini Zanzibar.

Kaimu Balozi Mdogo wa India Govind Sharan Gupta akiwahutubia wananchi mbalimbali wanaoishi Zanzibar waliohudhuria katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Jamuhuri ya India kuadhimisha miaka 67 katika ofisi za Balozi migombani Zanzibar. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.