Habari za Punde

Maandamano ya Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar Uwanja wa Amaan Zanzibar leo.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Abdalla Mwinyi Khamis na Meya Mstahiki wa Manispa ya Zanzibar Mhe Khatib Abduraham Khati wakiwa katika uwanja wa Amaan wakisubiri kuwapokea wageni waalikwa wanaohudhuria Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakisubiri kuwapokea Wakuu wa Serikali wakaati wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika viwanja vya Amaan Zanzibar leo asubuhi 12/1/2016
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume akiwasili katika viwanja vya Amaan Zanzibar kuhudhuria sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais Mstaaf Dk Mohammed Gharib Bilal akiwasili katika viwanja vya Amaan akipokelea na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Abdalla Mwinyi Khamis.
Mabalozi wa Nchi mbalimbali wanaowakilisha Nchi zao Tanzania wakihudhuria maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wananchi wakati alipowasili katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili katika Uwanja Amaan kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Amaan kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Amaan kuhudhuaria Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioadhimishwa leo katika viwanja vya Amaan Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akielekea kukagua Bwaride rasmin la Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akikagua bwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakisimama wakati wa kupigwa Wimbo wa Taifa.
Viongozi wa Jukwaa Kuu wakisimama wakati wa kupigwa Wimbo wa Taifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akirudi baada ya kukagua bwaride rasmin la sherehe za Mapinduzi kutia miaka 52 lililofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.