Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ziarani Kisiwani Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkurugenzi wa baraza la Mji Mkoani (kulia) Issa Juma Othman na kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla, wakishuka njia ya vidaraja wakati rais huyo akiitembelea
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohamed Shein, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa serikali wakati alipowasiliwilaya ya Mkoani Pemba, kukagua ujenzi wa njia za viadaraja na misngi ya maji ya mvua na ukarabati wa jengo la afisi ya Baraza la mji wilayani humo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk: Ali Mohamed Shein akiwa na mkandarasi wa ujenzi wa Chinjio lililopo Wesha Chake chake Elimeka A. Shuma akikagua ramani ya jengo hilo. 

 Mkurugenzi wa baraza la Mji Mkoani Issa Juma Othman akitoa maelezo ya ujenzi mitaro ya maji ya mvua kwa rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, wakati alipofanya ziara kuangalia kazi inavyokwenda
Mmoja kati ya mitaro minne iliojengwa na Baraza la Mji Mkoani kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa ajili ya kupitishia maji ya mvua, ambapo rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi dk Ali Mohamed Shein aliitembelea, (Picha nja Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.