Habari za Punde

Taasisi za kiislamu zashauriwa kuweka mfumo wa pamoja wa ukusanyaji Zaka na Sadaka

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
 Baadhi ya wanachama wa Jumuiya na wageni walikwa wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) hayupo pichani wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.

 Mgeni rasmin Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.

 Sheikh Ahmad Haydar Jabir akikumbusha juu ya kutoa Zaka na Sadaka, na kutofautisha baina ya Sadaka na Zaka, amewataka waumini kusoma kuyajua hayo.
 Mmoja wa waalikwa, Sheikh Said Khalid Said akichangia katika Mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya hiyo Dkt. Mohammed Hafidh akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza kwa Mkutano. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.  

Na Maelezo Zanzibar. 03/01/2016

Taasisi za kiislamu nchini zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kislam.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar, Sheikh Abdalla Talib amesema lengo la mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kusadia na kupunguza umasikini katika jamii lakini kwa sasa wengi wanaotoa sadaka hizo hazifikii lengo hilo kwa vile kumekosekana mfumo bora  unaowafikia watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa.


Akifungua mkutano wa Jumuiya ya Zaka na Zadaka Zanzibar, ZASA ametolea mfano wa nchi ya Denmark ambayo ina waislamu kwa asilimi 3 tu lakin imekuwa na utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa Sadaka na Zaka  hali iliyofanikisha kupatikana misaada mingi iliyosaidia  katika nchi hiyo na hata nchi nyengine.

Amefahamisha kuwa  kwa kuwa  Zanzibar asilimia kubwa ya wanananchi wake ni waislamu ina nafasi ya kufikia malengo hayo kama pia itatoa elimu kwa wananchi hasa wenye uwezo  ili kufahamu  umuhimu wa Ibada hiyo pamoja na njia bora za kutoa Zaka na Sadaka katika jamii.

Nae mwenyekiti wa Jumuiy hiyo, Sheikh Said Masoud  amesema kwa sasa umekuwa na mwamko mdogo hasa kwa wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka  kulingana na taratibu zinazotakiwa  kidini.

Nae katibu wa Jumuiya hiyo ya Jusaza, Omar Abubakar Mohamed amesema Jumuiya hiyo  imeshatoa Zaka kwa watu 46 zikiwemo za fedha taslim, charahani, friza na wengine kujengewa nyumba.            

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.