TANGAZO KWA WAFANYABIASHARA WOTE
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwatangazia
wafanyabiashara wote kuwa:-
1. Kwa wafanyabiashara ambao wanadaiwa kodi mbalimbali
wanakumbushwa kulipa haraka kwani kukaa na fedha ya serikali ni
kukosesha maendeleo ya Taifa letu na ni kitendo cha aibu. Tunawapongeza
walipakodi wote ambao wanalipa kodi kwa wakati.
2. Ni wajibu wa kila mfanyabishara kutoa risiti kwa mauzo yote
unayoyafanya. Pia wateja wote mnawajibu wa kudai risiti kwa manunuzi
yote mnayoyafanya ili kuchangia katika mapato ya serikali
3. Wafanyabiasha ambao wanafanya biashara bila ya kuwa na Namba ya
Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)) wafike katika ofisi za TRA ili wapatiwe
TIN. Kumbuka utaratibu wa kupatiwa TIN umeboreshwa na hutolewa
BURE.
4. Kwa wale wenye magari ya biashara (biashara za usafirishaji) wanasisitizwa
kuja kulipia kodi yao ya mapato (TRA) kwa mwaka 2016 kabla ya mwezi wa
Machi 2016 kumalizika.
5. Mwisho, Maofisa wa TRA watapita sehemu za biashara kwa lengo la
kuelimisha na kufuatilia wale wote wanakiuka sheria na taratibu za kodi.
Hivyo TRA inaomba ushiriano wenu ili kufanikisha zoezi hili.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu”
Imetolewa na,
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi
No comments:
Post a Comment