Habari za Punde

Umoja wa Maaskofu wakanusha kuhusika na barua ya Maalim Seif aliyomuandikia Papa Francis

 Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiwakaribisha viongozi wakuu wa  Umoja wa Maaskofu Zanzibar kuzungumza na waandishi wa Habari kupinga kuhusika  na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis, wakwanza (kulia) ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo Askofu Michael Hafidh na (kati) ni Katibu Mkuu Askofu Dickson Kaganga.

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dikson Kaganga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo  kukanusha kuhusika kwao na barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyomuandikia Papa Francis.
  Waandishi wa Habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Dickson Kaganga katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mnazimmoja.

Mwenyekiti wa Umoja wa Maaskofu Zanzibar Askofu Agostino Shao akijibu maswali ya  waandishi wa Habari  kwenye  mkutano wa kupinga kuhusika kwao na Barua ya Maalim Seif Sharif Hamad aliyompelekea Papa Fransis. (kushoto) ni Askofu Shayo na (kulia) ni Askofu Dickson Kaganga.

PICHA NA ABDALLA OMAR – HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.