Habari za Punde

ZLSC Pemba yafanya semina juu mafunzo kwa jumuia za vijana wa mkoa wa kaskazini Pemba, juu ya ulinzi wa haki za binadamu

 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa jumuia za vijana wa mkoa wa kaskazini Pemba, juu ya ulinzi wa haki za binadamu, kulia ni Afisa Mipango wa kituo hicho Khalfan Amour Mohamed, na kushoto ni mfanyakazi wa kituo hicho Asia Awadh, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WASHIRIKI wa mafunzo ya ulinzi wa haki za binadamu, ambao ni wanachama wa jumuia kadhaa za vijana za mkoa wa kaskazini Pemba, wakiwa makini kusiliza mada zinazowasilishwa, kwenye mafunzo yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 WASHIRIKI wa mafunzo ya ulinzi wa haki za binadamu, ambao ni wanachama wa jumuia kadhaa za vijana za mkoa wa kaskazini Pemba, wakiwa makini kusiliza mada zinazowasilishwa, kwenye mafunzo yalioandaliwa na kufanyika Kituo cha Huduma za Sheria ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mipango wa Kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, akiwasilisha mada juu ya dhana ya haki za binadamu, kwa wanachama wa jumuia za vijana za mkoa wa kaskazini Pemba, mafunzo hayo yameandaliwa na ZLSC, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MWANASHERIA wa serikali kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa mashitaka Pemba, Ali Bilali Hassan, akiwasilisha mada juu ya sheria ya mtoto no 6 ya mwaka 2011, kwa wanachama wa jumuia za vijana za mkoa wa kaskazini Pemba, mafunzo hayo yameandaliwa na ZLSC, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
KIJANA Mkasi Sharif kutoka wilaya ya wete, akisoma kazi za vikundi, kwenye mafunzo ya ulinzi wa haki za binadamu yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.