Habari za Punde

Uteuzi wa Naibu Gavana Benki Kuu ya Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi RAPHAEL, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi RAPHAEL alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. 

Ndugu Julian Banzi RAPHAEL anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.

Gerson P. Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU,
DAR ES SALAAM.

28/01/2016

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.