Habari za Punde

ZIRPP Monthly Lecture: "Uzanzibari, Utaifa na Usajili wa Ukaazi"

Chairperson: Mr. Muhammad Yussuf

Speaker: Ms. Salma Ahmed Maoulidi

Subject: "Uzanzibari, Utaifa na Usajili wa Ukaazi" (Zanzibariship, Nationality and Registration of Residents)

Date & Time: Saturday 30 January 2016; at 4:00 pm.
Venue: ZIRPP Office; Third Floor, behind Majestic Cinema 
(above ZANLINK)


Abstract:  Wakati wa duru ya mwisho ya vikao vya Baraza la Wawakilishi la Nane (2010-2015) baadhi ya wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) walilamikia utaratibu wa uandikishaji wa wapiga kura. Hatimaye katika kikao cha 28 aliyekua Waziri wa Kazi na Mawasiliano, Mheshimiwa Juma Duni Haji na ‘Chief Whip’, alitoa taarifa kuwa Mawaziri wa CUF katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa hawajaridhika na ‘utaratibu na uendeshwaji’ wa uandikishaji wa wapiga kura unaosimamiwa na Wizara ya Nchi, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ. Kutoridhika huku kulipelekea mawaziri pamoja na wajumbe wa CUF kutoka nje ya Baraza la Wawakilishi.

Hakika hii si mara ya kwanza kuwa suala la uandikishaji wa wapiga kura linazua mdororo wa kisiasa na hata wa kijamii katika visiwa vya Unguja na Pemba. Mbali na kuonekana kama ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Mzanzibari ya mwaka 1985 (Sheria Na. 5 ya 1985) kuna mtizamo ambao unahusisha kutungwa kwa sheria hiyo na suala zima la siasa visiwani Zanzibar, hususan udhibiti wa wigo la wapiga kura.


Kwa hivyo, mada itajaribu kuangalia suala la Usajili wa Wazanzibari Wakaazi katika muktadha mpana zaidi wa namna suala la utambulisho wa Mzanzibari linavyoakisi mabaki ya migongano, baadhi yakiwa ya kihistoria na baadhi yakiwa ni mazalia ya ushindani wa kisiasa katika mfumo wa kidemokrasia. Vilevile, mada itajaribu kumurika namna tafsiri juu ya ‘Uzanzibari’ na namna utambulisho huo unavyotunukiwa inavyoendelea kuigawa jamii ya Kizanzibari badala ya kuhimiza umoja wa kitaifa kama ilivyosisitizwa na waasisi mwaka 1964 na Katiba ya Zanzibar mwaka 2010.  

Lengo la uwasilishwaji wa mada hii si tu kutambua tu namna ilivyopitishwa Sheria ya Usajili wa Wazanzibari Wakaazi (Sheria Na. 7 ya 2005) na ilivyoleta hisia kali na kuzua mpasuko mkubwa katika jamii ya Kizanzibari, lakini pia kwa madhumuni ya kuuliza na kuibua maswali muhimu yatakayosaidia kuona zaidi ya kitovu finyu cha uchaguzi na kutafakari athari pana zaidi ya sheria zinazozonga ustawi wa demokrasia.

Mtoa Mada: Salma Maoulidi, kwa sasa Mjumbe katika mradi linganishi unaofuatilia maendeleo ya Uchaguzi, Siasa za Uchaguzi na Mabadiliko ya Kisiasa katika Kanda ya Afrika ya Masharaiki unaoratibiwa na Taasisi ya African Research and Resource Forum (ARRF).

Tea, Coffee and Snacks will be served freely.

Please forward this message to anybody who may be interested. Those who would like to attend should send their email addresses and telephone numbers to: zirpp@googlegroups.com.

Please confirm your participation.
All are welcome.

Muhammad Yussuf
Executive Director
Zanzibar Institute for Research and Public Policy
P.O. Box 4523, Zanzibar, Tanzania; 
Tel: +255 242 223-8474;
Fax: +255 242 223-8475; 
Cellular: 0777 707820;
Website: www.zirpp.info

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.