Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Masauni Atembelea Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kujitambulisha.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Masauni alipofanya ziara katika Jeshi hilo Zanzibar kujionea Utendaji wake akiwa katika ziara ya kujitambulisha.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake Zanzibar kujitambulisha kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi Zanzibar.kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame, mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.kabla ya kuaza ziara yake kujionea utendaji wa Jeshi hilo Zanzibar.
Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alipofika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa kujitambulisha. 

Makamanda wa Jeshi la Polisi Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alipofika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa kujitambulisha. 
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni, akiwa na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame, wakitoka katika jengo la Makao Makuu ya Polisi Ziwani kwa kuaza ziara yake baada ya mazungumzo na Maofisa hao.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.