Habari za Punde

Tangazo la Nafasi za Kazi ZSSF


MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
                                                                                                                  

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), umeanzishwa chini ya sheria nambari 2 ya mwaka 1998 ambayo ilifanyiwa mapitio makubwa na kuundwa upya sheria nambari 2 ya mwaka 2005. Bodi ya Wadhamini ndio chombo kikuu cha maamuzi na Mkurugenzi Mwendeshaji ndie msimamizi wa shughuli za kila siku za ZSSF.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar anakaribisha maombi kutoka kwa watanzania wenye sifa na uwezo  wa kujaza nafasi 4 za kazi kwa nafasi mbalimbali katika miradi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii.  Nafasi hizo ni kama ifuatavyo:

1.    FUNDI UMEME – NAFASI 1 (Unguja):

a)    UZOEFU WA KAZI:
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 5 katika fani hii.

b)   MAJUKUMU:
i)     Atawajibika kwa Mkuu wa kiwanja.
ii)    Atasimamia kazi zote zinazohusiana na chumba cha umeme (power house) ikiwa ni pamoja na usafi, matengenezo na ufanyaji kazi wa vifaa vyote vilivyomo katika chumba hicho.
iii)   Kushirikiana na shirika la umeme (ZECO) na kuhakikisha kuwa huduma ya umeme inapatikana katika kiwanja kwa muda wote wa kutoa huduma.
iv)   Kusimamia matengenezo ya vifaa vyote vya umeme vilivyopo katika kiwanja ikiwa ni pamoja na nyaya, taa na vifaa vyenginevyo.
v)    Kusimamia usomaji wa mita na kuhakikisha ulipaji wa malipo ya umeme unaotumika katika kiwanja.
vi)   Atakuwa na dhamana ya vifaa vyote vya umeme vilivyopo katika kiwanja.
vii) Kusimamia ufanyaji kazi wa vipoza hewa (AC) na kuhakikisha vinafanya kazi muda wote.
viii)                Kazi nyenginezo atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.


c)    SIFA ZA KIELIMU:
Awe na elimu ya ngazi ya Diploma katika fani ya Umeme kutoka Chuo kinachotambulika.

d)   MASHARTI YA AJIRA:
Ajira hii itakua ya mkataba wa muda wa miaka miwili (2).  Mkataba huo unaweza kuongezwa iwapo hali itaruhusu na pande zote mbili (2) zitakubaliana kufanya hivyo.

2) FUNDI BOMBA – NAFASI 2 (1 UNGUJA – 1 PEMBA)

a)    UZOEFU WA AJIRA:
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 5 katika fani hii.

b)   MAJUKUMU:
i)     Atawajibika kwa Mkuu wa kiwanja.
ii)    Atasimamia uendeshaji wa kila siku wa shughuli za bwawa la kuogelea ikiwa ni pamoja na matengenezo, kushughulikia watumiaji na kusimamia wasaidizi.
iii)   Kuhakikisha kuwa bwawa la kuogelea lipo katika hali nzuri ya usafi na kuridhisha wakati wote.
iv)   Kusimamia vifaa na samani zote zinazohusika na bwawa la kuogelea pamoja na vifaa vyote vya maji safi na maji taka.
v)    Kusimamia usafi na matengenezo ya bomba za maji safi na maji taka katika kiwanja.
vi)   Kusimamia utendaji kazi wa kisima na bomba za maji ya ZAWA, ikiwa ni pamoja na matengenezo.
vii) Kusimamia huduma ya maji ndani ya vyoo na sehemu zote zinazohitaji huduma hiyo.
viii)       Kushirikiana na Mamlaka ya maji (ZAWA) na kuhakikisha kuwa huduma ya maji inapatikana katika kiwanja kwa muda wote wa kutoa huduma.
ix)   Kusimamia usomaji wa mita na kuhakikisha ufanyaji wa malipo ya maji unaotumika katika kiwanja.
x)    Kazi nyenginezo atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

c)    SIFA ZA KIELIMU:
Awe na elimu ngazi ya Diploma au elimu ngazi ya Cheti katika fani ya Ufundi Bomba kutoka Chuo kinachotambulika.


d)   MASHARTI YA AJIRA:
Ajira ya mkataba wa kazi maalum kwa kipindi cha miaka miwili (2).  Mkataba huo unaweza kuongezwa muda kulingana na kazi zilizopo na makubaliano ya pande zote mbili (2).

3.) FUNDI ELEKTRONIKI – NAFASI 1 (Unguja)

a)    UZOEFU WA KAZI:
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 5 katika fani hii.

b)   MAJUKUMU:
i)     Atawajibika kwa Mkuu wa kiwanja.
ii)    Atakuwa msimamizi wa jengo la michezo ya video (Games Centre).
iii)   Atakuwa msimamizi wa vifaa vyote vya michezo ya video (video games) na kuhakikisha kuwa vinafanya kazi muda wote.
iv)   Kusimamia matengenezo ya vifaa vya michezo ya video.
v)    Kazi nyenginezo atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

c)    SIFA ZA KIELIMU:
Awe na elimu ya ngazi ya Diploma katika fani ya Elektroniki au ‘Computer Programming’ kutoka Chuo kinachotambulika.

d)   MASHARTI YA AJIRA:
Ajira ya mkataba wa kazi maalum kwa mujibu wa kazi itakayokuwepo kwa kuzingatia makubaliano ya pande mbili (2).  Mkataba huu utakua wa miaka miwili (2).

4.)  MSAIDIZI AFISA MANUNUZI, UGAVI NA UTAWALA: - NAFASI 1 (Unguja)

a)    UZOEFU WA KAZI:
Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka 3 katika fani hii.

b)   MAJUKUMU:
i)     Atawajibika katika manunuzi na utunzaji wa taarifa za kiwanja.
ii)    Atakuwa msaidizi katika kusimamia haki zote za wafanyakazi Kariakoo.
iii)   Atatunza mali na vifaa vyote vya Kiwanja cha Kariakoo pamoja na michezo ya video (video games) na kuhakikisha kuwa vinafanya kazi muda wote.
iv)   Atasaidia kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi na mali za Kituo.
v)    Kutekeleza majukumu na maelekezo kutoka kwa kiongozi wake.

c)    SIFA ZA KIELIMU:
Awe na Diploma katika fani ya Manunuzi na Ugavi kutoka Chuo kinachotambulika.

d)   MASHARTI YA AJIRA:
Ajira ya mkataba wa kazi maalum kwa mujibu wa kazi itakayokuwepo kwa kuzingatia makubaliano ya pande mbili (2).  Mkataba huu utakua wa miaka miwili

MSHAHARA:
Wale watakaofanikiwa katika maombi haya watapata malipo kwa mujibu wa kazi watakayofanya na kwa mujibu wa makubaliano au mkataba wa ajira.

MASHARTI YA KUOMBA NAFASI:
Muombaji lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 45.

Ombi liambatanishwe na cheti cha kuzaliwa, nakala ya vyeti vya masomo mbalimbali aliyosoma, maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu (3) wa kuaminika.

  1. Waombaji walioajiriwa wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  2. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  3. Mwisho wa kutuma maombi ni Ijumaa Februari 19, 2016.
  4. Barua za maombi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  5. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania ni lazima wathibitishe vyeti vya masomo TCU kabla ya kuomba ajira.
  6. Maombi yote yawasilishwe kwa mkono katika afisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii zilizopo Kilimani – Mnara wa Mbao kwa Unguja na Tibirinzi – Mguye kwa Pemba wakati wa saa za kazi kwa kutumia anuani ifuatayo:


MKURUGENZI MWENDESHAJI
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
P.O.BOX 2716
KILIMANI MNARA WA MBAO, ZANZIBAR

Na kwa Pemba

MKURUGENZI MWENDESHAJI
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR
P.O.BOX 296
TIBIRINZI CHAKECHAKE - PEMBA


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.