Habari za Punde

Tazama Daraja la Watembea kwa Miguu la Furahisha Jijijni Mwanza, Litavyokuwa Baada ya Kukamilika Kwake.

Baada ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kamera ya Binagi Media Group imenasa picha za daraja hilo litakavyokuwa baada ya kukamilika hivyo enjoy kuzitamaza na uvute picha namna Mwanza inavyoendelea kuboresha miundombinu yake.
Ukifika Mwanza, Make Sure unafika Rock City Mall Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.

2 comments:

  1. basss tutabaki kuwaangalia watanganyika tu wanavyojenga nchi yao, marikiti pale kinahitajika kitu kama hicho miaka nenda miaka rudi sasa serekali haijali kitu, siasa tu sisi inatia uchungu.

    ReplyDelete
  2. They are making progress and we are making politics

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.