Habari za Punde

Wagombea wa Chama cha ADC Zanzibar Wawakilishi na Madiwani Wathibitisha Kushiriki Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar March 20,2016.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Chama cha ADC Mhe. Khamis Mohammed akiwaonesha waandishi wa habari majina ya Wagombea wa Chama hicho waliohudhuria mkutano na kutowa maamuzi ya kushiriki kugombea Nafasi za Uwakilishi na Udiwani katika Uchaguzi wa Marudio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa marchi 20, akitowa maelezo hao kwa waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar huko Ofisini kwao Bububu Unguja. 
Kamishna wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wa Chama cha ADC Mhe. Juma Ali Khamis akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na kushiriki kwa wagombea wao katika uchaguzi wa marejio unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao Unaoshirikisha Nafasi za Urais wa Zanzibar Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wa Wadi Zanzibar. na kusema wagombea wao wako tayari katika uchaguzi huo.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa Chama cha ADC. 
Waandishi wakiwa makini kupata habari za kushiriki kwa Chama cha ADC katika chaguzi ya marejeo inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao wa marchi 20.
Wagombea wa Chama cha ADC wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari. 


1 comment:

  1. Hawa walipata kura ngapi uchaguzi ulopita?
    Tamaa mbele mauti nyuma

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.