Habari za Punde

Kina Bausi Waruhusiwa Kuwania Uongozi wa ZFA, Washindwe Wenyewe Tu.

Katika kuelekea kwenye mchakato wa uchaguzi wa viongozi watatu wa juu wa Chama cha Mpira wa miguu Zanzibar ZFA, ufafanuzi umetolewa kuingia hatua hiyo.




Makamu wa rais wa ZFA Pemba Ali Mohammed alisema hakuna kipengele chochote ndani ya katiba kinachomzuia Mzanzibar kutoingia katika hatua hiyo.

Ali alitoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa uvumi kwamba katiba ya chama hicho inamtaka yeyote anayehitaji kugombea nafasi hizo lazima awe ameshatumikia uongozi wa ZFA angalau kwa muda wa miaka minne.



"Si kweli hakuna kipengele kinachoelezea hivyo, mimi nasema akina kocha Bausi huu ni wakati wao kuja kugombea ili wapate ridhaa ya kubadilisha hali ya soka la Zanzibar".




Kiongozi huyo alisema tayari kamati itakayosimamia uchaguzi huo chini ya mwenyekiti wake Affan Othman Juma imeshapewa baraka na wanachosubiri ni bajeti ya kamati hiyo.




Wajumbe wa mkutano mkuu wa ZFA wanatarajiwa kuchagua rais wa ZFA taifa, Makamu wa rais ZFA Unguja na Pemba.




Kinyang'anyiro hicho kinatarajiwa kufanyika tarehe tisa mwezi ujao kisiwani Pemba ikiwa hakutokuwa na mabadiliko yoyote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.