Habari za Punde

Polisi Wafyatua Mabomu ya Machozi Mbele ya Benki ya CRDB, Tawi la Mbagala - Rangi Tatu, ni Kufuatia Ubishi wa Wateja Kutumia Simu Ndani ya Benki.



NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
POLISI wamelazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliojikusanya mbele ya Benki ya CRDB tawi la Mbagala-Rangi Tatu, baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiongea na simu ndani ya benki hiyo kukaidi maagizo ya polisi ya kuacha kufanya hivyo mapema leo mchana Machi 11, 2016.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, watu watatu mmoja akiongea na simu na wengine wawili waki-chat, ndani ya benki hiyo, waliagizwa na mlizni wa benki kuacha kufanya hivyo lakini wakakaidi.
Baada ya mlizni kuona hivyo alitoa taarifa kituo cha polisi Mbagala-Maturubai, na hapo polisi wakiwa ndani ya gari lao maarufu kama Defender, waliwasili kwenye eneo hilo na kuamuru watu hao ambao wanaelezwa kuwa wateja, kutoka ndani ya benki hiyo.
Hata hivyo palitokea mabishano baada ya mmoja wao kukaidi amri ya polisi na kuanza kupigana nao.
Kuona hivyo watu walianza kujaa na polisi bila kufanya ajizi wakafyatua mabomu ya machozi kutawanya watu na kuwadhibiti “wateja’hao wabishi na hatimaye kufanikiwa kuondoka nao.
Hali hiyo ilizua tafrani hadi watu wakadhani kuwa palikuwepo na tukio la ujambazi kwani ni mwezi uliopita umbali wa mita chache kutoka kwenye benki hiyo, palitokea tukio baya la uvamizi wa benki ya Access ambapo watu saba waliauawa wakiwemo polisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.