STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.3.2016
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan
Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza
la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa
uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55
(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo
ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi
Khamis.
Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan
Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa
Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi
wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment