Balozi wa Uturuki nchini Yesemin Eralp amezindua kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd.
Tukio hilo lilitokea jumamosi hii hapa jijini ambapo balozi huyo alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kujitokeza kuwekeza kwenye sekta hiyo.
Alisema kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vema kwenye sekta ya utalii huku ikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyovutia zaidi na kuwavutia watalii kutokea nchi mbalimbali.
Aliongeza kuwa wageni kutokea nchi mbalimbali duniani wanahitaji huduma kutokea kwa kampuni bora zaidi itakayowahudumia kwa ufanisi na umakini.
Kwa upande wake Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo Meysun Buyuksarac alisema kuwa kampuni hiyo imelenga kuimarisha utoaji bora wa huduma za usafiri wa ndege pamoja na utalii nchini.
Alisema kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za utalii ambapo zimekuwa zikipelekea wageni wengi kujitokeza kuja nchini kutalii, na hivyo kupekekea wageni kutokea nje ya kuja kwa wingi na wao kama kampuni wamejipanga kutoa huduma bora zaidi ili kukidhi uhitaji.
No comments:
Post a Comment