Habari za Punde

Uteuzi wa Mkapa Unatia Matumaini - BAN KI MOON

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,  akiwasilisha  mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,   taarifa yake kuhusu ziara yake aliyoifanya hivi  karibuni nchi Burundi. Katika  taarifa  yake  ameelezea kutiwa matumaini  matumaini na uteuzi wa Rais Mstaafu Mhe.Benjamin Mkapa  kuwa Mwezeshaji wa  majadiliano ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi  akizungumza kwa  niaba ya  Jumuiya ya Afrika  Mashariki katika mkutano  wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana  Ijumaa  kuhusu Burundi. Aliyeketi  nyuma ya  Balozi, ni  Bw. Khamis Abdallah  Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi, Bw. Alain Amic Nyamitwe naye akielezea hali ya mambo  na jitihada mbalimbali ambazo serikali ya Burudi imekuwa ikichukua katika kuresha hali ya amani na utulivu.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  katika mkutano wao wa Ijumaa ambapo baada ya  kupokea taarifa kuhusu Burundi,  waliendelea na kikao chao cha ndani.

Na MwandishiMaalum, New York                                                     
Wakati Mwezeshaji wa majadiliano kuhusu mgogoro wa kisiasan 

chini Burundi,  Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin 

William Mkapa akiwa ameanza mchakato wa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema, 

uteuzi wa   Benjamin Mkapa unatia matumaini.

Ban Ki Moon ametoa kauli hiyo jana Ijumaa, wakati alipokuwa 

akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa 

Mataifa,  taarifa kuhusu ziara yake aliyoifanya nchini Burundi 

mwezi uliopitia.

“Uteuzi uliofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 

wakumteua Rais Mstaafu wa Tanzania  Benjamin Mkapa kuwa 

mwezeshaji wa majadiliano kuhusu  Burundi  ni maendeleo 

yanayotia moyo”.Amesema  Ban Ki  Moon.

Na Kuongeza, ni lazima Jumuiya ya Afrika Mashariki, 

Umoja wa Afrika, Jumuiya na Umoj a wa Mataifa kusaidia 

utalamu wa hali ya juu wa usuluhishi ambao  Burundi  unahitaji.

Akielezea zaidi kuhusu ziara aliyoifanya nchi Burundi 

ziara iliyomwezesha kukutana na kufanyamazungumzo na 

Viongozi wa Kisiasa akiwamo Rais wa Nchi hiyo Bw. Piere 

NKurunzia. Ban Ki Moon, amesema hakuna njia mbadala zaidi ya mazungumzo ya kisiasa ambapo pande zinazopingana zitakaa katika meza ya mazungumzo.

Akasema,wakati wa ziara hiyo iliyofuatia baada ya wajumbe wa 

Baraza Kuu la Usalama kufaya ziara yao, alitoa wito kwa wadau 

wapande zote kutorejea kule walikotoka akimaanisha vita 

vilivyosababisha vifo vya wananchi wengi wa nchi hiyo kabla ya kupatikana kwa Mkataba wa Amani wa  Arusha ( The ArushaAgreement).

“Nilitoa wito kwa pande zinazopingana wananchi wa Burudi 

kutorejea kule walikotoka na kuonyesha dhamira ya dhati ya kukaa 

katika meza ya mazugumzo ya pamoja yakayokuwa na 

jumuishi na umoja wa kisiasa kwa kuwa hiyo ndiyo njia sahihi na 

pekee ya kutatua mgogoro wao“. Akasisitiza Ban Ki Moon.

Ban  Ki Moon ameelezazaidikuwaaliwaelezaviongoziwa  Burundi 

kwambakusainiwakwaMkatabawa Arusha Agosti 2000  

uliotokanamahasimukukaamezamojanakukaakatikamezanakukubali

anakumaliza vita  vyawenyewekwawenyewe pia 

ulifunguaukurasampyawamaridhianonakushirikianowakuijenganchi

yao.

AkabanishakuwaRaiswa Burundi  

wakatiwamazungumzoyaoaliahidikutekelezamambaokadhaayakiwa

koyakuwaachiahuruwafungwawakiwamoviongoziwaupinzani,  

kutoauhurukwavyombovyahabaripamojanakusitishavitendovyaukiu

kwajiwahakizabinadamunamauajiyaholela.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika 

Umoja wa Mataifa, akizugumza kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika 

Mashariki, ameliambia Baraza Kuu la Usalama kwamba, Rais wa 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe.  John Pombe Magufuli, 

kama Mwenyekiti wa EAC, anaamini kwa dhati kabisa kwamba  

hali ya kisiasa  nchini Burundi inaishughulisha siyo tu Ukanda wa 

Afrika ya Mshariki, bali pia    Jumuiya ya  Kimataifa.

“  Hali  ya Kisiasa inaishughulisha EAC na Jumuiya ya Kimataifa,  

siyo  kwa  sababu Burundi ni mwanachama wa EAC,  lakini ni 

kutokana na  ukweli kwamba  athari za mgogoro wa Burundi 

zinaweza kutuathiri sisi sote”. Akasema Balozi  Manongi  kwa 

niaba ya EAC.

Na kuongeza    ni  kwa kulitambua hilo ndiyo maana EAC 

inaendelea na juhudi zake za kutafuta suluhu  ya kudumu   nchini 

Burundi, na kwamba inakaribisha juhudi zinazofanywa na Katibu 

Mkuu wa Umoja wa Mataifa za kushirikiana na Burundi  na  

Kanda 

ya  Afrika Mashariki.

“Sisi kama Jumuiya ya Afrika Mashariki tunaomba juhudihizi 

tunazozikaribisha ziende sawia na  hatua za kuboresha na kusaidia 

mahitaji ya kijamii nakiuchumi ya watu wa  Burundi,  ikiwani 

pamoja na kuisaidia  kuimarisha  mifumo na  Taasisi zake za 

kiutawala.” Amesisitiza Balozi Manongi.

Msemaji   huyo wa EAC akabinisha kwa kusema , hapana shaka   

pana mambo mengi yanayochangia  uwepo  wa hali tete ya kisiasa 

nchini Burundi. Mambo anayosema yanapashwa  kujadiliwa wa 

uwazi na katika  ujumla wake. Na kwamba EAC  inawashukuru 

wale wote ambao wamekuwa wakiunga mkono jitihada 

zinazofanywa na EAC.

Akizungumzai kuhusu  utezi wa Rais Mstaafu  Benjamin Mkapa 

kuwa mwezeshaji wa  mazungumzo ya Burundi akimsaidia  Rais 

wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni,  Balozi Manongi amesema, 

EAC imetiwa na inashukuru kwa kauli za kutia moyo za kuukubali 

uteuzi wa Rais mstaafu Mkapa.

Akasema  katika  juhudi zake  za   kuisaidia Burundi nawatu wake 

alizofanya wakati wa mchakato wa  Amani wa  Arusha. Mkapa 

alisema yafuatayo

“ Suluhu endelevu kuhusu mgogoro wa Burundi unatakiwa kutoka  

ndani ya majadiliano ambayo wadau wote wenye dhamana 

kuhusu Burundi watashiriki kwa uhuru. Suluhu endelevu  

inatakiwa kumilikiwa na  kuheshimiwa  na washiriki wote wa mchakato wa  kutafuta amani. Shinikizo kutoka nje haiwezi kuleta suluhu ya kudumu”Balozi Manongi akabanisha kwamba  maneno hayo  aliyoyasema  Rais Mstaafu wakati huo  bado yana matinki na uzito   katika mazingira na hali ya sasa ya Burundi.

Na kuongeza ,  inatia moyo kuwa Rais Mstaafu Mkapa amekwisha 

anza ziara za awali za kuwatembelea viongozi na wadau mbalimbali  ndani ya EAC   kwa lengo la kuhakikisha kwamba  viongozi na wahusika wote  wanakuwa na uelewa wa pamoja kuhusu dhamana mpya aliyokabidhiwa.

Na  amewahakikishia viongozi wa EAC dhamira yake, kujituma kwake, uwazi na  ujumuishi katika  utekelezaji wa dhamana hiyo.

“Rais Mstaafu Mkapa anahitaji uungwaji mkono wa dhati na 

ushirikiano  kutokapande zote nchini Burundi,  katika EAC na 

katika Jumuiya ya Kimataifa” akasisitiza  Balozi Manongi.


Wengine waliotoa taarifa zao  kuhusu hali ya Burundi alikuwa ni  

Kamishna wa  Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa ya Haki za  

Binadamu  Prince Zeid Raad Hussein,  Mwenyekiti wa Burundi 

Configuration Balozi  Jurg  Lauber na Bw. Alain Amic Nyamitwe, 

Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa   wa 

Jamhuri ya Burundi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.