Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa Dawa Nasir Salum Buheti akiuliza swali na kutoa mchango wake katika mafunzo ya udhibiti wa Dawa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibae.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar ambae pia alikuwa mwenyekiti katika mafunzo hayo Dk. Burhani Othman Simai akiongoza mafunzo hayo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa Mafunzo ya siku tano ya udhibiti wa Dawa, yaliyoandaliwa na Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Fatma Kassim/Wizara ya Afya.
BODI ya Chakula Dawa na Vipodozi inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa Dawa zinazoingia nchini ni salama na zinafaa kwa matumizi ya mwanadamu.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zahran Ali Hamad wakati akifungua mkutano wa siku tano wa udhibiti wa dawa kwa wafamasia wa hapa nchini.
Amesema ni vyema wafamasia hao kutumia taaluma walinayo ili kuhakikisha wanadhibiti uingiaji wa dawa zisizo na viwango kwa lengo la kumkinga watumiaji na maradhi mbali mabali yanayotokana na dawa.
Amewataka wafamasia hao kuongeza jitihada katika suala zima la udhibiti wa dawa wakati zinapoingia nchini kwa kuwezesha kuepuka matatizo ya afya za wanaadamu.
Alisema hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni vyema kuongeza ushindani wa utoaji wa huduma bora kwa jamii na kuhakikisha kuwa Zanzibar haiingizi dawa bandia.
Mrajis wa Bodi ya Chakula Dawa na vipodozi Dk Burhan Othman Simai amesema kuwa katika mpango mkakati wao ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wake ili kuweza kukabilina na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni
Amefahamisha kuwa katika kukabilina na hali iliyopo hivi sasa ni vyema Serikali kuongeza wafanyakazi wa kada ya ufamasia ili kuweza kufanyakazi kwa ufanisi katika sehemu tofauti.
Alisema wataendeleza mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kwenda sambamba na haja iliyopo na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mapema mkufunzi wa usajili wa Dawa kutoka Mamlaka ya Chakula Tanzania David Robert Matle amesema ni vyema dawa kuifanyia usajili kwa kutimiza vigezo vya ubora, usalama wa dawa hizo.
Amesema lengo la usajili wa dawa ni kuwalinda wanaadamu wasipate madhara yanayotokana na dawa.
.
No comments:
Post a Comment