Habari za Punde

Athari za Mvua za Masika katika Maeneo ya Kwahani Uwanja wa Farasi Yakiwa Yamejaa Maji Kutokana na Mvua za leo.

Baadhi ya Nyumba katika eneo la Uwanja wa Farasi Unguja zikiwa zimejaa maji na wakaazi wa nyumba hizo kuhama makazi yao kutokana na kujaa kwa maji hayo. 
Wananchi wa Kwahani Uwanja wa Farasi wakihama maeneo yao baada ya nyumba zao kujaa maji kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika Visiwa vya Unguja.
Ngombe wakiwa katikati ya Uwanja wa Farasi wakizingirwa nma maji kutokana na mvua ya jana usiku kuamkilia leo kuwakuta wakiwa katika zizi lao na kushindwa kuondoka eneo hilo kutoka na kujaa kwa maji kama walivyokutwa asubuhi ya leo wakishangaa eneo hilo. 
Wakaazi wa uwanja wa farasi ilibidi kuhama makazi yao kutokana na nyumba zao kujaa maji ya mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar na kusababisha zaidi ya Nyumba 900 kuharibika na mvua hizo na wananchi wake kukosa mahali pa kuaa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.