Habari za Punde

Matukio Mitaani Zenj


Wananchi wakifuatilia mzozo kati ya mfanyakazi wa Manispa ya Zanzibar kitengo cha maegesho ya magari baada ya kulifungia gari lililoegesha eneo lisiloruhusiwa kando ya barabara ya darajani marikiti kuu. 
Baraza la Manispa Zanzibar likiwa katika jitihada za kupunguza msongamano wa magari katika eneo la Drajani hasa wakati wa mchana kwa baadhi ya Wananchi kuegesha magari yao kando ya barabara hiyo na kusababisha msongamano huo imechukua jitihada za kuweka alama za kuzuiya uegeshaji wa magari hayo kama inavyoonekana pichani muandishi akiandika bango la si ruhusa kusimamisha gari gari eneo hilo.

2 comments:

  1. Mizozo hii haitakwisha milele Zanzibar,Darajani ni eneo kuu la biashara,mipango miji yetu haikuzingatia kabisa suala la parking za vyombo vya moto. Hebu sasa tufikirie uwekezaji katika sekta hii ya parking za magari,hivi hatokezei mfanyabiashara mmoja akajenga jengo la kama ghorofa kumi hivi eneo la Vikokotoni ikawa ni kitega uchumi kizuri badala ya watu wooote kuekeza kwenye utalii tu. Hebu tuwe na ubunifu na tujaribu na eneo jengine la uwezekaji kama hilo la parking, definitely kuna soko la kutosha hapa mjini, kutokana na kutokuwepo kabisa kwa investment ya aina hiyo. Ningekuwa na uwezo mm ningefanya hiyo investment wallah

    ReplyDelete
    Replies
    1. Well said, very good idea, I appreciate it

      Delete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.