Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga
wakisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt.
Magufuli amesali ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa
Rais.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida
Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais Dkt. John
Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa katika kanisa la
Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Kikundi
cha Kwaya ya vijana wakiimba katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato
mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono kutakiana amani ya bwana na masista wa
kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida
Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko Padre Henry Mulinganisa katika ibada ya pili
ya pasaka Chato Mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko wa Parokia
ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa .
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato
mkoani Geita.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia
ya Chato mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia
ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amechangia kiasi cha Shilingi milioni
10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato
mkoani Geita.
Mkuu
mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria
Parokia ya Chato mkoani Geita.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida
Odinga pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia salamu zilizokuwa
zikitolewa na Raila Odinga katika kanisa
la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida Odinga
pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada ya ibada.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga wakiagana na waumini wa kanisa
la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sista Maria Theleza Ntihabose wa
kanisa la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment