·
Zachagua Wenyeviti
na wasaidizo wao
·
Machano, Dkt Mwinyihaji Kuongoza Kamati
Na,
Himid Choko, BLW.
SPIKA wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid ameunda Kamati saba (7) za
Kudumu za kisekta za Baraza la wawakilishi , ili kuhakikisha kwamba Baraza hilo linatekeleza kwa ufanisi mkubwa zaidi Kazi ya kuisimiamia serikali.
Katibu
wa Baraza la Wawakilishi Dkt Yahaya Khamis Hamad amesema Spika Maulid ameunda Kamati
hizo kwa mujibu wa Kanuni ya 107 (1) (a)
ya Baraza la Wawakilishi Toleo la 2012.
Amesema
kwa mujibu wa Kanuni hiyo mjumbe yeyote
wa Baraza asiyekuwa Makamu wa Pili wa Rais, Waziri, Naibu Waziri au Mwanasheria
Mkuu anaweza kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kudumu yeyote inayohusika na
Kanuni za Baraza.
Dkt
Yahya amezitaja Kamati hizo kua ni ile ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa
Kitaifa, ambayo itahusika na Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
pamoja na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. Wajumbe wa Kamati hii wamemchagua
Omar Seif Abeid ( Konde) kuwa Mwenyekiti na
Panya Ali Abdullah (Viti Maalum) kuwa Makamo Mwenyekiti.
Wajumbe
wengine wa Kamati hii ni Amina Idd
Mabrouk (Viti Maalum), Mtumwa Suleiman Makame (Viti Maalum) , Simai Mohammed
Said (Tunguu) , Mohammed Said Dimwa (Mpendae), Hussein Ibrahim Makungu (Mtoni) na Mussa Ali Mussa (Ole) . Awali katika Baraza
lililopita Kamati hii ilikua ikiongozwa na Hamza Hassan Juma akiwakilisha Jimbo
la Kwamtipura.
Kamati
nyengine ni ya Sheria na Utawala, ambayo inahusika na Ofisi ya Rais, Katiba, Utumishi wa Umma na
Utawala Bora na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na
Idara Maalum za SMZ ambapo wajumbe wa Kamati hiyo wamemchagua aliyewahi kuwa
Waziri na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi katika awamu zilizopita Machano Othman Said (Mfenesini) kuwa
Mwenyekiti wake na Mwantatu Mbarak
Khamis (Viti Maalum), kuwa Makamo
Mwenyekiti.
Wajumbe
wengine wa Kamati ya Katiba Sheria na Utawala ni pamoja na Saada Ramadhan Mwenda
( Viti Maalum), Wanu Hafidh Ameir (viti Maalum), Mihayo Juma N,hunga (Mwera),
Shamata Shaame Khamis ( Micheweni), Nadir Abdullatif Yussuf (Chaani) na Ali
Khamis Bakari(Tumbe).
Dkt.
Yahya amesema aliyekuwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa katika Awamu iliyopita ,
Hamza Hassan Juma (Shauri Moyo) ameendelea kutumikia wadhifa huo katika Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ambayo itahusika na Wizara ya Ardhi , Maji,
Nishati na Mazingira pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji .
Amesema
Kamati hiyo ya Mawasiliano na ujenzi pia imemchagua Suleiman Sarhan Said
(Chakechake) kuwa Makamo mwenyekiti wake . Wajumbe wengine wanaounda Kamati
hiyo ni pamoja na Mohammedraza Hassanali
Mohammedali (Uzini), Abdullah Ali Kombo (Mwanakwerekwe), Mwanaidi Kassim Mussa
(viti maalum), Khadija Omar Kibano (Mtambwe), Bahati Khamis Kombo (Chambani),
Nassor Salim Ali (Kikwajuni), na Said Omar Said (Wingwi),
Kamati
nyengine ni Kamati ya Maendeleo ya wanawake na Ustawi wa Jamii ambayo imemchagua aliyekuwa Waziri katika
Awamu zilizopita Dr. Mwinyihaji Makame (Dimani)
kuwa Mwenyekiti na Tatu Mohammed
Ussi kuwa Makamo Mwenyekiti wa kamati
hiyo.
Wajumbe
wengine wa Kamati hii ambayo itahusika
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na Wizara ya Afya ni Viwe Khamis
Abdullah( Viti Maalum), Hidaya Ali Makame ( Viti Maalum), Mwanaasha Khamis Juma
( Chukwani) , Masoud Abrahman Masoud ( Bububu) , Ame Haji Ali ( Nungwi) na
Makame Said Juma (Kojani).
Kwa
upande wa Kamati ya Kuchunguza na
Kudhibiti Hesabu za Serikali na Mashirika (PAC) inaongozwa na Miraji Khamis
Mussa (Chunbuni) na Makamo Mwenyikiti wake
ni Shaib Said Shaib (Chonga) , Wajumbe wengine ni Mtumwa Peya Yussf (Bumbwini), Zainab Abdullah
Salum (Viti Maalum), Dr. Makame Ali Ussi( Mto pepo), Abdullah Maulid Diwani Jang”ombe), Zulfa
Mmaka Omar (Viti Maalum).
Kamati
ya Fedha, Biashara na Kilimo inayohusika na Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara
ya biashara, Viwanda na Masoko pamoja na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi inaongozwa na Yussuf Hassan Idd (
Fuoni ) na Makamo mwenyekiti wake ni Hamida Abdullah Issa ( Viti Maalum).
Wajumbe wengine wa Kamati hii ni Ussi Yahya
Haji (Mkwajuni), Bihindi Khamis Hamad (Viti Maalum), Shadya Mohammed
Suleiman ( Viti Maalum) , Ali Salum Haji (Kwahani), Hamad Abdullah Rashi(Wawi),
na Mohammed Mgaza Jecha( Mtambile).
Dkt
Yahaya ameitaja Kamati ya mwisho kuwa ni ile ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na
Habari itakayohusika na Wizara ya
Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Kazi, Uwezeshaji , Wazee
, Vijana , Wanawake na Watoto. Amesema kamati hiyo itaongozwa na Ali Suleiman
Ali( Kijitoupele) na Makamo Mwenyekiti wake ni Salha Mohammed Mwinjuma (Viti
Maalum).
Wajumbe
wengine ni Zainab Abdullah Salum ( Viti
Maalum), Asha Abdullah Mussa (Kiwengwa), Jaku Hashim Ayoub( Paje), Suleiman
Makame Ali (Ziwani), Mussa Foum Mussa( Kiwani), Hassan Khamis Hafidh ( Welezo)
na Maryam Thani Juma (Gando).
Mwisho
Imetolewa
na Divisheni ya Itifaki na Uhusiano, BLW
O777436016.
Sunday,
17 April 2016
No comments:
Post a Comment