Habari za Punde

Taasisi ya Ikhlas Charitable Group Zanzibar Yakabidhi Msaada kwa Wananchi Waliopata Maafa ya Mvua Zanzibar.

Mwakilishi wa Taasisi ya Ikhlas Charitable Group Ust Mohammed Suleiman (Tall) akitowa maelezo kwa niaba ya Taasisi yao wakati wa kukabidhi vyakula kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed kwa ajili ya Wananchi wanaokaa katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja baada ya makaazi yao kuingiliwa na maji ya Mvua za Masaki. hafla hiyo imefanyika katika Kambi hiyo ilioko Skuli ya Mwanakwerekwe C Zanzibar. 
Mwakilishi wa Taasisi ya Ikhlas Charitable Group Zanzibar Ust Mohammed Suleiman (Tall ) akimkabidhi msaada wa Vyakula Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed. 
Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed, akitowa shukrani kwa Taasisi ya Ikhlas Charitable Group Zanzibar kwa msaada wao kwa Wananchi waliopata maafa ya Mvua za Masika zinazonyesha katika Visiwa vya Zanzibar.
Vyakula na bidhaa zenyine zilizotolewa na Taasisi ya Ikhlas Charitable Group Zanzibar vikishushwa baada ya kukabidhiwa kwa wahusika katika kituo cha Skuli ya Mwanakwerekwe Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.