Wanafunzi wakichuana katika mchezo wa netball wakati wa bonanza la Halotel lililofanyika katika viwanja vya Mabibo Hostel
Wanafunzi wa Chuo kikuu Dar es Salaam wakipambana na wanafunzi wa chuo cha ualimu (DUCE) wakati wa bonanza la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
Msanii Msami akitoa burudani wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo.
Mkurugenzi wa Halotel tawi la Dar, Bwana Alex Thiem akizungumza na wanafunzi wakati wa Bonanza la Halotel lilifanyika viwanja vya Mabibo Hostel
Msanii Ruby akiburudisha wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
Stamina akiburudisha wanafunzi wakati wa tamasha la Halotel lililofanyika Mabibo Hostel.
Baadhi ya
wanafunzi waliohudhuria tamasha la Halotel katika viwanja vya Mabibo
Hostel.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni ya simu Halotel juzi ilizikonga nyoyo za wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia tamasha lake la ‘Back to University’ lililofanyika katika Viwanja vya Hostel ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wanafunzi.
Tamasha
hilo lilipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi
kipya, Msami, Ruby na Stamina pia lilitawaliwa na michezo ya aina mbalimbali
kama vile Netiboli, soka na mingineo.
Akizungumzia
kuhusiana na tamasha hilo Mkurugenzi wa Halotel tawi la Dar es Salaam, Bwana
Alex Thiem alisema tamasha hilo lina lengo la kuimarisha uhusiano baina ya
Halotel na wanafunzi wa vyuo vikuu.
‘Toka
mtandao wetu umeanza hapa nchini tumejikita katika kuhakikisha tunaboresha
huduma za simu nchini, lakini kwa upekee kabisa tumekuwa tunawapa wanafunzi
huduma bora na nafuu zaidi’ alisema bwana Thiem
Kwa
upande wa burudani Msami alipopanda jukwaani alitumia takribani dakika 45
kuzikonga nyoyo za mashabiki wake hao ambapo aliimba nao na kucheza pia hasa
akionesha umahiri wake wa kucheza dansi.
Naye
msanii Ruby anayetamba na kibao chake kipya cha Forever, alitoa burudani kali
kwa maelfu ya wanafunzi waliojitokeza katika hosteli hizo.
Ilipofika
majira ya saa 12 jioni akapanda jukwaani msanii Stamina ambae ameandika historia
ya kipekee kwa wanafunzi hasa kwa aina yake ya uimbaji wa mashairi yaliyokuwa
yakishangiliwa mara kwa mara.
Tamasha
hilo lilianza majira ya saa nne asubuhi kwa michezo ya aina mbalimbali kama
vile Netiboli pamoja na soka ambapo katika mchezo wa Netiboli timu ya wanafunzi
wanaume iliibuka na ushindi wa mabao 11 - 10 dhidi ya timu ya wanawake.
Kwa
upande wa mchezo wa soka zilicheza timu mbili ambapo ilianza timu ya Baraza la
Mawaziri la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya
timu ya Idara ya Mazoezi ya Viungo.
Katika
mechi nyingine, timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ikaifunga timu ya
Chuo Kikuu cha Ualimu (DUCE) 1-0.
Michezo
hiyo kwa ujumla ilizokonga nyoyo za wanafunzi wengi ambapo pia walipata wasaa
wa kujiunga na huduma za mtandao huo wa simu kama vile kununua laini, kujiunga
vifurushi na mengineo.
Kwa
upande wake waziri wa michezo wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam, bwana Jackson Mayunga aliishukuru kampuni ya Halotel kwa kufanikisha
tamasha hilo.
‘Tunawashukuru
sana Halotel kwa kufanikisha tamasha hili, na kama unavyoona wanafunzi wamepata
nafasi ya kuburudika lakini pia kubadilishana mawazo’ alisema Mayunga.
No comments:
Post a Comment