GARI za abiria zikiwa zimesongamano
katikati ya mji wa Chakechake, baada ya wamiliki wa gari hizo kudai, kutekeleza
agizo la serikali ya mkoa wa kusini Pemba, la kuzitaka gari hizo, zishushe na
kupakia abiria kwenye egesho kuu ‘stand’ badala ya kutumia zile za zamani
zilizopo pembezoni mwa mji huo (Picha na
Habiba Zarali, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:
Mwanajuma Majid Abdalla na kushotoni kwake Katibu tawala wa mkoa huo, Ahmed
Khalid na Kamanda wa Polisi wa mkoani humo Shehan Mohamed Shehan wakienda
kwenye egesho kuu la gari za abiria, ili kutoa ufafanuzi baada ya kutokezea
vurumai kwa gari za abiria kuweka msururu mrefu ndani ya mji wa Chakechake, (Picha na Habiba Zarali, Pemba).
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:
Mwanajuma Majid Abdalla, akizungumza na vyombo vya habari, mara baada ya
madereva kudai kutii agizo la serikali ya mkoa, kuziingiza gari zote kwenye
egesho kuu jambo lilizoua vurumai jana majira ya asubuhi, (Picha na Habiba Zazrali, Pemba).
No comments:
Post a Comment