Mkuu wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) Omar Mwalimu Omar akitoa elimu kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki juu ya njia bora za kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ikiwa ni maadhimisho ya siku ya afya Duniani.
Mkufunzi kutoka kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) cha Wizara ya Afya Rabia Ali Makame akifundisha wanafunzi wa Skuli ya SOS kuhusiana na visababishi vinavyopelekea maradhi yasiyo ya kuambukiza katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afya Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya SOS wakimskiliza kwa makini Mkufunzi kutoka kitengo cha maradhi yasiyoambukiza (NCD) cha Wizara ya Afya Rabia Ali Makame (hayupo pichani) wakati wa sherehe za siku ya Afya Duniani zinazoadhimishwa kila ikifika tarehe 7 kila mwaka.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment