Habari za Punde

Zanzibar yazindua wiki ya chanjo Afrika huko Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja

KATIBU  Tawala wilaya ya Kaskazini B Juma Abdalla Hamad akitoa  maelezo  namna  wilaya ilivyojiandaa  kufanikisha uzinduzi wa  wiki ya chanjo Afrika katika sherehe ziliofanyika  kituo cha afya Kitope.
Wananchi mbali mbali waliojitokeza katika kuitikia wito wa siku ya chanjo Afrika katika uzinduzi uliofanyika  kituo cha afya Kitope.
KIKUNDI cha ngoma za asili cha Magereza kikitoa burudani katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo Afrika.

MKUU wa wilaya ya Kaskazini B Haji Makungu Mgongo akimkaribisha Naibu waziri wa afya Harusi Said Suleiman kuzindua  wiki ya chanjo Afrika.


NAIBU Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akiwahutubia wananchi mbalimbali wliohudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika kituo cha afya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.


Baadhi ya watoto waliojitokeza  katika maadhimisho hayo wakisubiri huduma ya chanjo.

Naibu  Waziri wa afya akizindua Rasmi  wiki ya chanjo Afrika kwa kumpatia tone la chanjo mtoto Mudrik Ali Khamis mkaazi wa  Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.(PICHA NA ABDALLA OMAR HABARI MAELEZO ZANZIBAR.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.