WAFANYAKAZI wa Wizara ya Biashara na Viwanda na Masoko Pemba,
wakizichana pakiti 204 za sukari iliyopitiwa na muda wakati wa uteketezaji wa
sukari hiyo huko katika mashimo ya makaani Vitongozi, sukari iliyokuwa
ikimilikiwa na Mfaranya biashara maarufu chake chake Mohamed Ali Aboud,(Munauwari)(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BAADHI ya wafanya biashara kisiwani Pemba, wamebuni ujanja wa
kuzibadilisha tarehe za kuharibika bidhaa zao, kama zinavyoonekana katika picha
Mfuko wa Super Special kahawa ikiwa imebadilishwa muda wake halisi wa mwisho wa
matumizi.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
KATIBU tawala Wilaya ya Chake Chake Rashid Abdalla Rashid, akiwa
ameshikilia baadhi ya soda soda zilizopitiwa na Muda, wakati wa kuvibagua
biadhaa hizo kabla ya kuchomwa moto huko Makaani Vitongoji Wilaya ya Chake
Chake. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
GARI aina ya Buldoza la Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, kikichanganya sukari iliyoharibika na mchanga, ili kuzuwia
wananchi wasiweze kuichukuwa ikiwa imeshapitiwa na muda, kazi hiyo iliyofanyika
huko Makaani Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
GARI aina ya Buldoza la Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Usafirishaji Pemba, kikichanganya sukari iliyoharibika na mchanga, ili kuzuwia
wananchi wasiweze kuichukuwa ikiwa imeshapitiwa na muda, kazi hiyo iliyofanyika
huko Makaani Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BAADHI ya wafanyakazi wa Wizara ya Biashara Viawanda na Masoko
Kisiwani Pemba, wakiimimina karafuu mbovu ambayo imeshapitiwa na muda, wakati
wa uteketezaji wa vyakula vibovu huko makaani Vitongoji Wilaya ya Chake Chake
Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
BAADHI ya bidhaa za majimaji kama vile Juisi, arki, marashi na
bidhaa za vitafunio vikiwa vimeshapitiwa na muda wake wa matumizi vikisubiri
kuteketezwa kwa moto huko Makaani Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba. (Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Hakuna njia ya mbadala ya kuziteketeza hizo bidhaa.
ReplyDeleteUchomaji hauathiri avya ya binadmu kutokana kemikali zilizotengezea vifungio kama hiyo mifuko na kadhalika