Habari za Punde

Kampuni ya Huawei yaungana na Watengenezaji mashuhuri wa kamera duniani; Leica kutengeneza simu P9



Bw. Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania.


               
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
29 Aprili 2016                                          Dar es Salaam

Mkakati wa Huawei katika kubadili namna uonavyo dunia iliyokuzunguka
Kampuni ya Huawei yaungana na Watengenezaji mashuhuri wa kamera duniani; Leica kutengeneza simu P9

Mwezi Aprili, Huawei wamezindua simu iliyokua ikisubiriwa kwa muda mrefu katika mlolongo wao wa simu zao za P Series; Huawei P9. Uzinduzi wa Huawei P9 umezingatia kipaumbele cha teknolojia ya hali ya juu. Toleo hili la tisa la P Series limewezeshwa na Kampuni ya Huawei pamoja na kampuni mashuhuri kwa utengenezaji wa camera duniani Leica. Simu hii ina kamera ya kipekee yenye lenzi mbili, ambayo imeweka rekodi katika teknolojia ya kamera za simu za kisasa, ikiwa na mwanga Zaidi na ubora Zaidi, kupata picha zenye rangi nzuri Zaidi katika staili ya Leica ya kipekee.

Watanzania wanategemea kupata simu hii yenye teknolojia ya hali ya juu na ya kipekee katika kamera hivi karibuni. Hii inafuatia uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika mji wa Dubai wiki hii. Uzinduzi huo wa kipekee ambao ulihudhuriwa na viongozi wa Huawei Tanzania na Waandishi wa Habari umeashiria upatikanaji wa simu hii katika soko la Tanzania hivi karibuni.

Tokea uzinduzi wake mji wa London, simu hiyo imepata mapokezi makubwa kama simu “inayobadili namna uonavyo dunia”. Simu mpya ya kipekee Huawei P9 ina malengo kubadili ubora wa picha unaopatikana katika timu za kisasa maarufu kama “smartphone”. Teknolojia katika simu hiyo inabadili namna tunavyopiga na kufurahia picha, hii imetokana na shauku ya Huawei kuendelea kuvuka mipaka ya uvumbuzi, ikilinganishwa na uzoefu na kipaji katika utengenezaji wa kamera na lenzi wa Leica pamoja na ushirikiano mzuri katika kutengeneza P9.

Waliokuwepo katika uzinduzi huo ni pamoja na viongozi wakuu wa Huawei Tanzania akiwemo Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania, Lydia Wangari Meneja Masoko kampuni ya Huawei Tanzania, waandishi wa Habari na wadau mbalimbali kutoka Tanzania.


Akionglea ujio wa simu hiyo katika soko la Tanzania Bwana Huziangyang Jacko, Meneja wa Huawei nchini Tanzania alisema ”Tunategemea kuleta simu mpya ya Huawei P9 kwa wateja wetu wa Tanzania hivi karibuni; Tunaamini teknolojia hii ya hali ya juu na ya kipekee iliyotokana na utafiti wa hali ya juu na shauku ya kubadili namna watumiaji wetu waonavyo dunia inayo wazunguka, P9 ikifanya kazi na Leica, tumeweza kufanya maajabu katika teknolojia ya lenzi ya kamera”.

Akiongea katika uzinduzi huo, Lydia Wangari Meneja Masoko Huawei Tanzania alisema, ”Tunaendelea kuzindua simu mpya , tukitilia mkazo katika teknolojia ya kipekee. Kwa kushirikiana na wadau wengine, tumeweza kujumuisha utamaduni, mtindo ya maisha ya wateja wetu na teknolojia ili kuwapatia wateja watu simu bora zaidi”.

Kuongezeka kwa aina mbalimbali za simu za mkononi za smartphone nchini Tanzania inaashiria ukuaji na umuhimu wa Tanzania katika soko duniani huku wa Tanzania Zaidi wakigundua umuhimu wa teknolojia maishani mwao. Mahitaji katika maendeleo na simu za  kiteknolojia yanaongezeka kila kukicha nchini Tanzania na kampuni ya Huawei imeendelea kutatua hitaji hilo nchini Tanzania.

Kufuatia mafanikio ya simu aina ya P zijulikanalo kama “P Series”, kwa ujumla mapokezi ya simu ya Huawei P9 ni mazuri duniani kote. Huawei Tanzania wana matarajio makubwa juu ya ufanyaji kazi wake katika soko la Tanzania. Wakiahidi watumiaji simu yenye nguvu na ubora wa kipekee usio linganishwa, simu mpya ya P9 itapatikana katika rangi nne: Dhahabu, kijivu, Dhahabu iliyoiva Zaidi na Siliva huku P9 Deluxe Version ikipatikana katika rangi ya dhahabu na Nyeupe.

Familia ya simu za Huawei P9  imetumia njia za kipekee na ubora wa hali ya juu kubadili namna tunavyoona dunia iliyotuzunguka. Inaendeleza heshima ya Huawei ya simu zenye ubora wa juu ambazo zimeacha alama katika soko kwa ubora na ufanisi.
Huawei itaendelea kukamata fursa mbalimbali ili kubadili soko na kuinuka duniani katika biashara za watumiaji wa simu za mkononi. Huku simu za kampuni hiyo zikizidi kua na teknolojia ya hali ya juu, Huawei itaendelea kutengeneza vifaa vinavyoweza tumika na mteja wakati wowote na mahali popote. Na Wataendelea kuungana na wadau wengine katika soko la vifaa, programu. Kupitia uvumbuzi wa teknolojia pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali, kampuni ya Huawei ina ahidi kuleta vifaa Zaidi kwa wateja wake wote duniani.

Kuhusu Huawei

Huawei ni vinara wa teknolojia na mawasiliano hususani katika kutimiza matakwa ya wateja wao, katika kuhakikisha wanawapa wateja wao kile kilicho bora katika viwango vya juu, umuhimu wa mawasiliano na vifaa vya mawasiliano vinatumika katika nnchi Zaidi ya 170 na mikoa yake, Huawei ilishika nafasi ya 228 ulimwenguni kwa mwaka kutokana na mapato yake mwaka 2014 kati ya makampuni 500. Mapato ya kampuni yamefikia kiasi cha dolla za kimarekani bilioni 46.5. Huawei imeshika nafasi ya 3 kwenye usambazaji wa simu kwa mwaka 2015 kwa kusambaza zaidi ya simu milioni 100 duniani kote, Kampuni ya Huawei ipo katika kuhakikisha inatoa ushirikiano katika kukuza na kuboresha vifaa vya mawasiliano  duniani kote.

Kampuni ya Huawei inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi, huduma za intaneti kwa njia ya modemu na vifaa vya matumizi ya nyumbani.

Huawei imeimarisha mahusiania ya biashara na makampuni kama Tigo, Vodacom, Tigo, Vodacom, Airtel, Zantel, Sasatel, TTCL, SmileCom, Safaricom, MTN, CellC, Telefónica, China Mobile, Vodafone, T-Mobile, BT, China Telecom, NTT Docomo, France Telecom, na China Unicom.
Kupata habari Zaidi tembelea www.huaweidevice.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.